Ama kwa
hakika sio wote waishio baharini ni samaki, bwana Whether Brent Crawford amekamata
samaki ambao hafahamiki mwenye ana paund 300 na kuvunja historia ya muonekano
na kuzua gumzo namna anavyoweza kumudu uzito wake
Bwana Crawford alikua
katika maeneo ya Texas' na alimvua samaki huyo katika ziwa Corpus Christi ni miongoni mwa watu wachache waliowahi kuvua
samaki mwenye uzani mkubwa kama huo
Crawford, ameishi karibu na ziwa hilo kwa takriban muiaka
20 sasa alitaarifiwa na dada mmoja
aliyekua akiogelea kwenye ziwa hilo akiwa na vijana wengine watano ambao ni wadogo kua kuna jisamaki lisilokua la
kawaida kwenye ziwa hilo
baada ya ndoano kutupwa ziwani, mtupo mmoja tu akamchoma
sehemu ya kichwani jisamaki hilo, mara waya ukajizunguusha mkononi ,ukaanza
kumbanda mvuvi huyo ,na wakati
akitahayari, akavutwa mtoni akitanguliza kichwa mtoni .kumbe si mkono tu bali
hata mguu wake ulifungwa na mshipi wa kuvulia ,na ndipo mbwa wa mvuvi huyo
aitwae Bleux, akaanza kuvuta suruali
yake sehemu ya mguuni na kuzua mvutano wa ajabu kati ya samaki na mbwa
huyo mtoni .
lakini baadaye Crawford alifanikiwa
kuupachua mkono wake ,purukushani hiyo ilidumu kwa muda wa dakika 45 anaeleza
Crawford, alipoponyoka katika mtego huo aliichukua simu yake ambayo aliiweka
kwenye kifuko kisicho ingia maji na kumpigia rafikiye , ambaye alikuja na
bastola, na kumvuta samaki huyo kwa kamba na kumkokota hadi nyumbani kwa
Crawford.
No comments:
Post a Comment