Monday, August 13, 2012

NUKUU- TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU









                                   FAUSTIN MUSA


                                     SAMSON RAMADHANI


Ndoto za wanamichezo wa Tanzania kurudi nchini na medali toka kwenye michezo ya olimpiki zimefifia baada ya wanariadha FAUSTIN MUSA na SAMSON RAMADHANI kushindwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya marathon yaliyofanyika Jana huko jijini London.
FAUSTIN MUSA alishika nafasi ya 33 huku mwenzie SAMSON RAMADHAN akimaliza kwenye nafasi ya 66 .
Katika mashindano hayo mwanariadha toka UGANDA, STEPHEN KIPROTICH alifanikiwa kutwaa medali ya dhahabu baada ya kumaliza mbio hizo ndani ya muda wa masaa mawili  dakika nane na sekunde moja mbele ya wanariadha toka KENYA, ABEL KIRUI na WILSON KIPROTICH walioshika nafasi ya pili na ya tatu kwa mpangilio.

                    STEPHEN KIPROTICH

Medali aliyotwaa STEPHEN KIPROTICH ndiyo medali pekee ambayo Taifa la UGANDA limeweza kutwaa kwenye michezo ya olimpiki mwaka huu huku Kenya wakiwa wamekusanya jumla ya medali 11  ambapo medali mbili ni za dhahabu , nne za shaba na tano za fedha.





No comments:

Post a Comment