Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana akihakiki kama maji yanatoka!
haya sasa kazi kwenu, maji ndo haya tunakutwisha!
PAMOJA NA HAYO!MKWARA MZITO UMECHIMBWA
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Jaqueline Liana amempa saa 24 Mkuu
wa Idara ya Maji wa wilaya hiyo kuwasilisha ripoti ya mradi wa maji uliojengwa
katika Kijiji cha Bugabu uliofadhiriwa na kampuni ya Alpha Choice ya
Mwanza.
Amri hiyo ya Liana
inatokana na malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Bugabu wakati wa uzinduzi wa
mradi huo wa maji uliogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi million 5.Akizungumza
muda mfupi baada ya kuzindua mradi huo wa maji utakaosaidia wananchi wa vijiji
vitatu,
Jaqueline Liana amesema kumekuwa na tabia kwa wakuu wa idara
na viongozi wa vijiji kutosoma mapato na matumizi ya miradi.Amesema kuwepo kwa
usiri katika miradi mbalimbali kunawafanya wananchi kuichukua serikali yao,kitu
ambacho kinaweza kuepukwa iwapo suala la kusomwa mapato na matumizi
litazingatiwa.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Bugabu Rebecca Jonas na baadhi
ya wananchi wa kijiji hicho wamezungumzia changamoto mbalimbali kuhusiana na
mradi huo wa majiMeneja mauzo wa Kampuni ya Alpha Choice inayomiliki viwanda
vya kusindika minofu ya samaki katika nchi za Afrika Mashariki Bruno Mhoja
amesema mradi huo wa maji ni makakati wa kampuni kushirikiana na jamii katika
miradi ya maendeleo.Mradi huo wa maji ni wa kwanza katika kijiji cha Bugabu
kutolewa na wawekezaji ambao utawanufaisha
wananchi zaidi ya laki moja
No comments:
Post a Comment