
Hamza Bendelladj baada ya kukamatwa na polisi mjini Bengkok
Mshukiwa
mmoja wa udakuzi wa komputa ambaye anasakwa na idara ya ujasusi nchini
Marekani, FBI, kuhusiana na madai ya kuiba mamilioni ya madola kutoka benki za
Marekani, ili kufadhili maisha ya anasa, amekamatwa mjini Bangkok Thailand.
Shirika hilo
la FBI, limekuwa likimsaka mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24, Hamza
Bendelladj, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya komputa, kutoka Algreia kwa zaidi
ya miaka mitatu.
Ripoti
zinasema mshukiwa huyo amekuwa akiiba kutoka benki hizo za Marekani tangu
alipokuwa na umri wa miaka 20.Polisi nchini Thailand wanasema mshukiwa huyo,
Bendelladj amekiri alitumia fedha hizo kuisha maisha ya starehe na anasa.
Bendelladj,
anazuiliwa katika kituo kimoja cha polisi katika uwanja wa ndege mjini Bangkok
baada ya kuwasilia kutoka Malaysia akiwa safirini kuelekea Misri.
Utawala wa
Marekani unamtuhumu kuhusika na wizi katika akaunti za watu binafsi katika
zaidi ya mabenki 217 na taasisi wa kifedha kote duniani na kusababisha hasara
ya mamilioni ya madola.
Mkuu wa
polisi nchini Thailand amesema mshukiwa, alikamatwa katika uwanja mkuu wa ndege
ambako alisema yeye pamoja na familia yake wamekuwa likizoni.
Polisi
wanasema wamenasa komputa mbili, kifaa kimoja cha tarakilisha, simu ya sate
lite na vifaa vingine vya komputa kutoka kwa mshukiwa huyo.Ripoti zinasema
Bendelladj anatarajiwa kusafirishwa hadi nchini Marekani, katika Jimbo la
Georgia ambako mahakama moja ilitoa kibali cha kukamatwa kwake.
ndelladj
anatarajiwa kusafirishwa hadi nchini Marekani, katika Jimbo la Georgia ambako
mahakama moja ilitoa kibali cha kukamatwa kwake
No comments:
Post a Comment