Hii ni moja kati ya
zile kesi za kanisa katoliki zilizodumu kwa muda mrefu kesi ilianza toka mwaka 2007 ambapo serikali ilitishia kulifungia gazeti la
kanisa katoliki endapo lingeendelea
kumuita Mungu Allah.
Brazilian pop singer
Cláudia Leitte,JL na Pitbull walifanya show moja kali mno ambapo JL alitupa
shida na stress zake nyuma na kurusha mikono juu, akatisha mno na kivazi chake.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed
Gharib Bilal akiwa na Rais mpya wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya rais mpya wa Malawi kukabidhiwa madaraka leo
jijini Brantyre kwenye hoteli Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata
fursa ya kuzungumzia masuala la kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na
kukubaliana kuendelea kuwa na mahusiano mema kama nchi zinazoishi ndugu na
jirani. Picha kwa Hisani ya Ikulu ya Malawi
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mradi wa mafunzo ya bure kwa waandishi wa habari kwenye maeneo matano, sekta ya uchimbaji, unyanyasaji wa kjinsia, kupamba na biashara ya madawa ya kulevya na kuzuia utumiaji wa madawa ya Kulevya kwa waandishi wa habari na utayarishaji na utengenezaji wa vipindi vya luninga na wanawake watangazaji jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Msaidizi wa Mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya watu, Dorothy Temu –Usiri na Mkurugenzi wa Mfuko wa vyombo vya habari, Ernest Sungura.
Wasichana
wa Kimasai kutoka kijiji cha Ayamango kata ya Gallapo wilaya ya Babati
wakihudhuria mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana alipotembelea mkoa wa Manyara hivi karibuni.
Donald Sterling
amefungua kesi akiwashitakiNBA, na huku
akitaka alipwe fidia ya Dola Bilioni moja. Kwa madai kwamba kuzuiwa kwake
kuendelea kuwa mmiliki wa TEAM ni kunyume na katiba ya NBA.. Pia madai mengine
aliyoyafungua ni kupinga kulipishwa FINE ya Dola milioni mbili na nusu kwa
UBAGUZI..!!
Mwanamke aliyeasi dini
nchini Sudan na kupata adhabu ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela
mjini Khartoum kwa mujibu wa wakili wake.
Meriam Yehya Ibrahim
Ishag, aliolewa na mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo
kuhukumiwa kifo mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena.
Makamu wa Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uturuki, Ahmet Dovutoglu, aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo, Mei 30, 2014. Katika mazungumzo yao walisisitiza juu ya ushirikiano katika Nyanja mbalimbali baina nchi hizi mbili . Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki.