
Mwanamke aliyeasi dini
nchini Sudan na kupata adhabu ya kifo amejifungua mtoto mvulana akiwa jela
mjini Khartoum kwa mujibu wa wakili wake.
Meriam Yehya Ibrahim
Ishag, aliolewa na mwanamume mkristo jambo lililopelekea mwanamke huyo
kuhukumiwa kifo mapema mwezi huu baada ya kukataa kusilimu tena.

Ataruhusiwa
kumnyonyesha mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu kutekelezwa.Meriam aliyezaliwa na
wazazi waisilamu, alihukumiwa na mahakama ya ya kiisilamu.
'MIJELEDI MIAMOJA'
Bi Ibrahim alihukumiwa kifo kwa kosa la zinaa kwa sababu ameolewa na mwanamume mkristo wa kutoka Sudan Kusini na kwamba ndoa yao haikubaliki chini ya sheria ya kiisilamu ambayo inasema kuwa mwanamke musilamu hawezi kuolewa na mwanamume mkristo.
Kwa kosa hilo, jaji alimuhukumu adhabu ya mijeledi miamoja, adhabub ambayo itatelezwa pindi mama huyo atakapopata nafuu kutokana na kujifungua.
Bi Ibrahim alilelewa
kwa njia ya kikristo , dini ya mamake kwa sababu babake aliyekuwa muisilamu
hakuwepo katika maisha yake tangu utotoni.
Kwa mujibu wa shirika
la kimataifa la Amnesty International, alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la
Zinaa mwezi Agosti mwaka 2013, na mahakama ikamuongezea kosa la kuasi dini
Februari 2014 aliposema kuwa yeye ni mkristo wala sio muisilamu.
Sudan ina idadi kubwa ya waisilamu ambao wanafuata sheria za kiisilamu.
No comments:
Post a Comment