Tuesday, October 16, 2012

TATHMINI YA UMOJA WA MATAIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO


Balozi wa  Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Tuvako  Manongi, akizungumza  siku ya  Jumatatu,wakati wa Uzinduzi wa Tathmini ya Miaka  Minne ya Shughuli za Maendeleo za Umoja wa Mataifa ( QCPR). Uzinduzi ambao umefanyika  wakati wa Mkutano wa Baraza la Uchumi na Fedha  ( ECOSOC)la Baraza Kuu la 67 la  Umoja wa Mataifa. Tanzania ni Makamu Mwenyekiti wa  Baraza hilo.   Katika mchango wake Balozi aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili hali halisi ya  matatizo ya kiuchumi , kuongezeka kwa umaskini na upunguaji wa misaada ya  kimaendeleo  kwa nchi  hasa  zinazoendelea na  nafasi ya  Umoja wa Mataifa katika  ufadhili na usimamiaji wa miradi ya mendeleo  badala ya nchi wanachama kutumia muda mwingi kujitafutia uhalali na umaarufu. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Katibu  Mkuu, Bw. Jan Eliasson.

Friday, October 5, 2012

CHRIS BROWN ASIKIA KILIO CHA RIRI



Chris Brown ameonekana akiwa katika uwanja wa ndege wa Los Angeles ... na inadhaniwa amepungua kama 90 pounds. Hivi! Na hiyo inatanguliwa na tamko alilolitoa muda mfupi tu kua amemuacha girl friend wake Karrueche Tran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wake wa kirafiki na Rihanna Baada ya tamko hilo Karreuche na ulimwengu wanaamini kwamba Chris Brown na RiRi walikua na mahusiano ya kisirisiri.





DUNIANI WAWILI WAWILI, NIMEAMINI! BONGO TUMETISHAJE?




 


Rick Ross wa Bongo kumpokea airport Rick Ross wa Marekani, ama kweli duniani wa wili wa wili


Thursday, October 4, 2012

WATANZANIA SASA KUPATA BIMA KUPITIA M-PESA





·        Ni ushirikiano kati ya Vodacom na Heritage Tanzania kuzindua bima ya Faraja, Bima ya mazishi na ajali.Wateja kununua na kulipia Bima kupitia M-Pesa.
·
·    Huduma ya bure kutolewa kwa wateja watakaolipia huduma mara kumi kwa Mwezi.
Dar-es salaam, Octoba 3, 2012 … Huduma ya Vodacom ya M-Pesa imezidi kupiga hatua baada ya kuwawezesha Watanzania kufanya malipo yao ya bima kupitia huduma hiyo.
Hii inafuatia ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na Heritage Tanzania kuzindua Bima ya Faraja, ambayo ni Bima ya mazishi ambayo inamuwezesha mlengwa kulipwa fedha taslim za mazishi kwa muhusika mwenye bima. Bidhaa mbalimbali ziko katika mpango huo ili kukidhi mahitaji ya wateja na bajeti ya malipo ya kila mwezi kuanzia shilingi 20000/= fadi 9800/= kwa Mwezi.
Mteja ana chaguo la kuongeza malipo kwa kuongeza huduma ya vifo vinavyotokana na ajali kulingana na faida na sera zao. Ongezeko hili la ziada litaongeza kiasi cha faida mara tatu kwa ongezeko dogo la malipo.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa, wataweza kujipatia bima ya bure kwa mwezi.
“Wateja wetu wote ambao watafanikiwa kutuma pesa walau mara 10 kwa Mwezi watapata  bima ya bure ya kiasi cha Shilingi laki mbili kwa mwezi unaofuata,” amesema Meza.
Suala la kipekee katika huduma hii ni kwamba hakuna haja ya kujaza fomu ili kujiunga na bima hii. Mteja atajiunga kwa njia rahisi kwa kupiga *150*00# na kuchagua kipengele cha bima. Vodacom inahakikisha kuwa wateja wote wa M-pesa wanaweza kupata huduma hii ili kuwa na amani ndani ya familia zao.
 “Ni muhimu kuthibitisha kuwa taarifa zako ni sahihi, na kuthibitisha kuwa unaelewa vigezo na masharti. Taarifa zako zitatumwa moja kwa moja kwenda Heritage Tanzania,” alisema Meza na kuongeza kuwa, “Unaweza kuchagua aina ya bima ambayo inakidhi mahitaji na bajeti yako,”
Bima hii ya Faraja pia itawawezesha kila mmoja kubadili au kuongeza kiwango chake kwa ile yenye faida zaidi kulingana na mahitaji yao na mabadiliko ya bajeti katika maisha yao.
Kwa taarifa zaidi kuhusiana na huduma mteja atapiga 0764 300001 bure au vipeperushi kutoka kwa wakala wa M-Pesa nchini.
Mwisho … ///


FIESTA DAR-ES-SALAAM HAH MAANDALIZI YANAENDELEA!!!





Nilipotembelea viwanja vya Leaders Club hapa jijini Dar-Es-Salaam , kwenye harakati za kuangalia vitu kwa jicho la tatu nilikuta mambo yanaendelea kama yalivyo pangwa, nikakuta vitendea kazi viko eneo la tukio tayari kabisa kuusimika muonekano mpya lakini burudani ileile! Hah!





Jukwaa limeanza kupata muonekano huu, baada ya kuunga unga vyuma , likitayarishwa kwa ajili ya mnyama! The big boss himself Rick  Ross kukwea October 6 mwaka huu! , tel your friend , tel your Friend hah! Muonekano mpya burudani ni ile ile. Ticket utazipata hapa Clouds House, Escape 2 , Robby One Fashions, Born to Shine Mwenge karibu na TRA na kwingineko, huko utapata tiketi kwa tshs kwa 20,000/- na ukija mlangoni ni tshs 25,000/- kwa Serengeti Fiesta Bhaaaas! Usisite njoo na rafikiyo to parrrrtyy!!


Tuesday, October 2, 2012

BUSU HUONGEZA AFYA YA MWILI! NDIYO!

                               

                   Kiss with red lips

HIZI NI FACTS JUU YA BUSU  NA NAMNA YA KUBUSU !
Kwa kawaida huwa tunatumia misuli miwili tu ya uso tunapotoa busu kwa rafiki ama mzazi, lakini linapokuja suala la kumbusu mpenzi ama mume basi huwa tunatumia misuli yote ya uso kumbusu umpendaye nah ii husaidia kuunguza calories nyingi zaidi wakati wa busu kwa mpenzi!

Monday, October 1, 2012

FIESTA 2012 MPANGO MZIMA - THE BOSS



Alipewa jina hili na wazazi wake William Leonard Roberts II tarehe yake ya kuzalizaliwa inatajwa kama January 28, 1976, lakini katika majukwaa ya muziki anafahamika kama known by Rick Ross mara zote akalipa swag jina hilo la kazi as RICK RO$$, akiwa anapeperusha bendera kama  ni rapper wa  Kimarekani. Ross alivumbua record label Maybach Music Group, huko akatoa album yake iitwayo Deeper Than Rap mnamo mwaka 2009 na  album ni  Teflon Don ya 2010. Mwanzoni mwa mwaka huu wa 2012, MTV  ilimtambulisha Ross kama  Hottest MC In The Game.