Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA
Tanzania,Aldo Mfinde wakati alipokuwa akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar tayari kwa Uzinduzi rasmi wa maonyesho ya VICOBA Tanzania.Wa pili
Kulia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga na Kulia ni
Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa Simba.
Mratibu wa Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo
Mfinde akizungumza machache wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Maonyesho ya Miaka
Kumi ya Wafanya biashara ndogo ndogo na Wajasiliamali wa VICOBA
uliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.wa Tatu kulia
ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa.Wengine ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh.
Makongoro Mahanga (pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM,Wilaya ya Ilala,Mh Assaa
Simba.
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akimpongeza Mratibu wa
Maonyesho ya VICOBA Tanzania,Aldo Mfinde mara baada ya kumaliza kuitambulisha
Kamati ya VICOBA Tanzania iliokuwepo viwanjani hapo.
Burudani ya Ngoma za
Asili.