
Oscar Pistorius hayuko hali nzuri kiakili kushiriki mwaka 2013
Mshindi wa dhahabu wa mbio za
walemavu Oscar Pistorius hatashiriki katika mashindani yeyote mwaka huu kwani
anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake ya mauaji.Pistorius, mwenye umri wa miaka 26,
ambaye yuko nje kwa dhamana ameshitakiwa kwa kumuuwa mpenzi wake Bi Reeva
Steenkamp, hajakatazwa na waandalizi kushiriki mbio zozote.
Wakala wake , Peet van Zyl, amesema
mshindi huyo wa mbio za walevamu za Olimpiki mara sita hali yake ya kiakili kwa
wakati huu bado haimruhusu kushiriki katika amshindano yeyote."Mimi na hata kocha wake(Ampie
Louw) hatujawahi kumshinikaza aanza kushiriki mashindanoni, ni uamuzi wake yeye
mweyewe," amesema Van Zyl.
Pistorius alikamatwa tarehe 14
Februari mwaka huu baada ya kumpiga risasi na kumuua Bi Steenkamp na tangu
wakati huo haja shiriki katrika mashindano yeyote.Mwanariadha huyo amekanusha kosa la
mauaji na anadai kwamba alimpiga mpenzi wake risasi kimakosa kwani alifikiria
ni jambazi aliyekuwa amevunja nyumba yake.
Tarehe 22 Februari Pistorius
aliachiliwa kwa dhamana na kuondolewa vikwazo ambavyo vingelimzuia kushiriki
katika mashindano ya riadha.
No comments:
Post a Comment