MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA BUGANDO NA KUZINDUA JENGO LA MATIBABU YA UGONJWA WA SARATANI NA HUDUMA ZA UPASUAJI WA MOYO, MKOANI MWANZA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kushoto)
akishuhudia zoezi la upasuaji wa Moyo alipokuwa akifanyiwa mmoja wa wagonjwa wa
Moyo ndani ya Hospitali ya Bugando, baada ya kuzindua Jengo la Matibabu ya
Ugonjwa wa saratani na Huduma za Upasuaji wa Moyo, mkoani Mwanza wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Sikukuu ya
Bugando, iliyofanyika leo Hospitalini hapo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua
rasmi Jengo la matibabu ya Ugonjwa wa Saratani na Huduma za upasuaji wa Moyo
Shughuli ya Upasuaji
mgonjwa wa Moyo ikiendelea.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwajulia hali baadhi ya
wagonjwa kati ya watoto 18 waliokwishafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya
Bugando kwa gharama ya SH. 50, 000/ badala ya gharama sahihi ya Sh. milioni 6.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal
(katikati) akionyeshwa moja ya mashine zinazotumika wakati wa upasuaji wa Moyo
katika Hospitali ya Bugando.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia
wafanyakazi wa Hospitali ya Bugando, wakati wa sherehe za maadhimisho ya
Sikukuu ya Bugando 'Bungado Day'
No comments:
Post a Comment