Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Nchi kavu
na majini( Sumatra) Mkoani Mbeya imesitisha utoaji wa leseni ya kubeba abiria wa
kawaida kwa waombaji wapya wenye magari yenye uwezo wa kubeba abiria wasio zidi
14
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Athumani
Diwani
Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa
Nchi kavu na majini( Sumatra) Mkoani Mbeya imesitisha utoaji wa leseni ya kubeba abiria wa kawaida kwa waombaji wapya wenye magari
yenye uwezo wa kubeba abiria wasio zidi
14.
Aidha Mamlaka hiyo imesema kuwa endapo wamiliki hao
wa magari hayo watahitaji kutoa huduma kwa jamii mamlaka hiyo itatoa leseni kwa ajili ya kubeba watalii tu .
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya
na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Ndugu Diwani Athumani wakati akizungumza na
madereva wa mabasi madogo yaendayo Mji mdogo wa Tunduma Wilayani kufuatia kuwepo kwa mgomo uliodumu kwa miezi
3 sasa ambao umefanywa na madereva hao kwa
kuto safirisa abiria waendao Tunduma.
Mgomo huo wa
madereva hao umesababishwa na baadhi ya wamiliki wa magari madogo aina ya(
Noah) ambayo yamekuwa yakifanya shughuli ya kubeba abiria toka Mbeya hadi
Tunduma hali iliyo zua mgogoro mkubwa baina ya wamiliki wa gari hizo Ndogo
pamoja na madereva wa Costa ambao ndio wenye leseni za kusafirisha abiria Toka Mbeya hadi Tunduma.
Awali wakati akizungumzana madereva hao
Kamanda Diwani amewataka mara moja watu wanaofanya biashara hiyo kuacha mara
moja kwani sheria itachukua mkondo wake.
Amesema sababu kubwa ya kusitisa
huduma inayo tolewa na magari hayo madogo ni kuzuia majanga ambayo yanaweza
kutokea kwani gari hizo hazina madirisha makubwa pamoja na milango yake kuwa
midogo ambayo na haina milango ya dharura endapo kunaweza kutokea tatizo
lolote.
Kufuatia
hali hiyo Kamanda Diwani amewataka madereva costa ambao wamekuwa wakitoa
huduma hiyo kwa muda mrefu kuachana na
mgomo huo badala yake waendelee kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyo kuwa awali.
No comments:
Post a Comment