
Kwetu sisi hapa Tanzania kutokana na mila na desturi huwe kumkuta mwanamke anaanika tumbo ama ujauzito wake nje ,Na hata kama mwanamke huyo akiwa mjamzito akiwa kaolewa, kwake ni aibu watu wakijua? na ukijua ukamwambia we una mimba? atakuchukia na kukununia muda wote wa mimba mpaka mtoto!
Kisirani cha mimba bado sijakipatia picha! ni vijitabia vya ajabu ajabu sana, tena vya mpito lakini ni kiboko! sasa wenzetu huko mbele wao huona fahari kupata ujauzito, na maandalizi ya kuubeba huwa yanasemwa mapemaaa! na ikithibitika kua mwanamke ni mjamzito, yeye mwenyewe atakua wa kwanza kuwatangazia ndugu jamaa na marafiki kua ana tegemea mtoto"shes pregnant"! na asemapo husema kwa raha zote! tofauti na kwetu, mnuno mwanzo mwisho!






Kwa wale ambao huwa wananuna, mi hujiuliza, je umelazimishwa? kua na raha, maana kuitwa mama si kitu kidogo, na ni fahari kubwa! haya kwa wewe unaye tarajia mtoto, nakutakia kila la kheri wakati wote wa ujauzito wako.
No comments:
Post a Comment