ZIARA YA WAZIRI MWAKYEMBE NA BALOZI WA JAPAN
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Bw. Masaki
Okada (kushoto) akifurahia jambo na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison
Mwakyembe(mwenye suti nyeusi) ndani ya Behewa la Treni ya Dar es Salaam ,wakati
Balozi huyo alipotembelea Shirika la Reli Tanzania(TRL) na pia kutembelea eneo
la reli lililoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe
akipanda kwenye kiberenge kuelekea kwenye eneo la Tabata Mwananchi lililoharibiwa
na mvua kubwa zinazoendela kunyesha jijini Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi na
Balozi wa Japan nchini Tanzania walitembelea eneo hilo leo asubuhi ya jana kuangalia
maendeleo ya ujenzi wa eneo hilo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Balozi wa Japan
Nchini Tanzania, Masaki Okada.
Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison
Mwakyembe,akitoa ufafanuzi wa uharibifu uliotokea kwa Balozi wa Japan Nchiini
Tanzania,Bw. Masaki Okada.
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Bw. Masaki Okada
akishuka kwenye kiberenge, mara baada ya kumaliza ziara ya kuangalia eneo
lilihoribiwa na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha
usafiri wa treni ya Dar es Salaam kusimama. Akiongozana na Waziri wa
Uchukuzi,Dkt Harrison Mwakyembe.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya
Tanzania na Zambia (TAZARA), Dkt. Damas Ndumbaro(Kulia) anaemaliza muda wake ,
akitoa maelezo kwa Balozi wa Japan Tanzania, Bw. Masaki Okada (mwenye tai ya
njano) na Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia), wakati Balozi huyo
na Waziri wa Uchukuzi walipofanya ziara kujionea maendeleo ya usafiri wa Treni kwa Upande wa TAZARA .
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya
Tanzania na Zambia (TAZARA) anaemaliza muda wake, Dkt. Damas Ndumbaro(Kulia),
akitoa ufafanuzi wa ratiba ya treni ya TAZARA inayofanya safari zake kutokea
Stesheni ya TAZARA kwenda Mwakanga , kwa Balozi wa Japan nchini Tanzania
(mwenye tai ya njano), wakati alipotembelea Stesheni hiyo jana asubuhi.Balozi huyo
aliongozana na Waziri Mwakyembe katika ziara hiyo.
No comments:
Post a Comment