
Mke wa Rais, Jakaya
Kikwete, Salma, akionyesha Tuzo ya Heshima iliyotolewa na Falme za Kiarabu Dar
es Salaam, jana.
Rais Jakaya Kikwete, ameondoka nchini kwenda
Marekani kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Taarifa ya Ikulu kwa
vyombo vya habari jana, ilisema kuwa Rais Kikwete aliondoka juzi Jumatano na
kwamba kulingana na ratiba ya uchunguzi wa afya yake anatarajiwa kurejea nchini
Alhamisi ya wiki ijayo.
Hata hivyo, taarifa
hiyo iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, haikueleza bayana tatizo
linalomsumbua Kikwete mbali ya kusisitiza kuwa amekwenda huko kwa ajili ya
uchunguzi wa kitabibu.
Taaarifa za hali ya
afya ya Rais Kikwete kwa mara ya kwanza ilitolewa mwaka 2009, ikiwa ni siku
chache tu baada ya kushindwa kukamilisha hotuba aliyokuwa akiitoa kwenye
sherehe za miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Rais Kikwete
alilazimika kukatiza hotuba yake na kwenda kwenye chumba cha mapumziko kwa muda
wa dakika 10 kutokana na kile kilichoelezwa na daktari wake kuishiwa nguvu.
Wakati huohuo, Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete amewasili nchini jana akitokea Dubai, Falme za Kiarabu
ambako alipata Tuzo ya Dunia ya Hamasa ya Uongozi (Global Leadership
Inspiration Award), ambayo msingi wake ni kutambua uongozi madhubuti na hamasa
katika kutetea hadhi ya wanawake duniani.
Akizungumza tuzo hiyo
alisema: “Tuzo niliyopata ni heshima kubwa kwa wanawake wa Tanzania...hakuna
maendeleo ya kweli na endelevu bila wanawake, hivyo lazima jitihada zifanyike
kushirikisha wanawake katika sekta mbalimbali za maendeleo.” Mama Kikwete
aliwataka wanawake nchini kujitokeza kuzungumzia unyanyasaji wa kijinsia
wanaofanyiwa na wanaume.
No comments:
Post a Comment