WAZIRI WA UCHUKUZI, DK. HARRISON MWAKYEMBE AFUNGA MWAKA KWA KUWATAMBULISHA RASMI KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU KATIKA UKUMBI WA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM
Sehemu ya Watendaji wakuu
wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi na wafanyakazi wa Wizara hiyo
wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Shaaban Mwinjaka(Hayupo
pichani) wakati wa mkutano maalum wa kufunga mwaka na kuwatambulisha rasmi
viongozi hao uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe akiongea na wafanyakazi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizo
chini ya Wizara hiyo leo jioni katika mkutano maalum wa kufunga mwaka na
kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Shaaban Mwinjaka(kulia kwa
Waziri Mwakyembe)na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mrs Monica
Mwamunyange(kushoto kwa Waziri Mwakyembe Katika ukumbi wa Karimjee,jijini Dar
es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Uchukuzi, Mrs Monica Mwamunyange akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa
kufunga mwaka na kuwakaribisha rasmi Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu huyo.
Mkutano huo umefanyika leo jioni katika ukumbi Karimjee jijjini Dar es Salaam. Aidha
Naibu Katibu Mkuu huyo amesisitiza ushirikiano na kujiwekea malengo katika
utendaji kazi wa kila siku.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.
Shaaban Mwinjaka(wa kwanza kulia mstari wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Mrs Monica Mwamunyange(wa pili kutoka kushoto mstari wa kwanza) na wakuu
wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa
Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi
zilizo chini ya Wizara pamoja na Wafanyakazi wa WIzara hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Dk. Shaaban Mwinjaka(wa tatu kutoka kulia mstario wa kwanza), Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Mrs Monica Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto mstari wa
kwanza) na baadhi ya watumishi wa Wizara
ya Uchukuzi leo jioni katika Mkutano maalum wa Waziri wa Uchukuzi kuwatambulisha
rasmi viongozi hao kwa Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na
Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment