
Wamama na Wadada,
Kwanza nawape salamu za Mwaka mpya.
Pili: Natumai kuwa huu
ujumbe utakukuta u katika njema pamoja na familia yako. Kwa muda mrefu yumekuwa tukiandaa ama
kuhudhuria sherehe mbali mbali za ufundaji a.k.a kitchen party.
Ila swali ni hili: Hizi
shughuli ama mkusanyiko kiukweli haswa, zimesaidia kuponya nyumba zetu? Maadili
yetu, Fikra zetu bila kuathiri IMANI yetu mbele ya MUUMBA wetu? Hapa kuna
mwanya ama tatizo ambalo Ladies yatupasa kusaidiana kimawazo. Hivyo tukutane
Tarehe 8, Februari 2014.
Tutachangishana kiasi
cha Tzs. 30,000 kwa ajili ya vitafunwa
na vinywaji kiasi. Ukumbi, ni free maana
kuna mkereketwa ameamua kujitolea. Siku ya siku tutaambizana mengi ikiwamo uboreshaji wa Forum hii, na pia kuipa jina
mkusanyiko huu, jina lenye Mvuto, Siha na Maudhui.
Kwa Mawasiliano zaidi
wasiliana na Janeth 0754 24 8080
Na kwa Watsup tu:
0767024262
Mchoro wa Eneo utatumwa
siku zikikaribia.
No comments:
Post a Comment