

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, wakitoa heshima za miwsho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu George John Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili huo zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, akielekea kutoa heshim za mwisho.

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, Makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi, wakishiriki Misa maalum ya kumuombea marehemu John Liundi, wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu na Bunge) William Lukuvi (kushoto) wakitafakari msiba huo wakati wa shughuli za kuagwa mwili zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

Sehemu ya wanafamilia wakishiriki shughuli hiyo.



Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Makamuwa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif, baada ya shughuli za kuagwa mwili wa marehemu Lindi, zilizofanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam

No comments:
Post a Comment