Monday, January 6, 2014

RAIS KIKWETE NA MAKAMU DKT. BILAL WAWAONGOZA WANANCHINKUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. MGIMWA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR.




Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,. Mwili huo umesafirishwa  kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko. 





Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilala, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, janamchana. Mwili huo umesafirishwa  kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.




 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
Mama Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho.
Mawaziri wakibeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. William Mgimwa wakati likipakiwa kwenye gari tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa ndege kuelekea mkoani Iringa kwa maziko.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, heshima za mwisho.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwa katika shughuli hiyo.
Baadhi ya Mawaziriki wakiwa katika foleni kuelekea kutoa heshima zao za mwiho.

 Mwili ukipakiwa kwenye gari.

No comments:

Post a Comment