Thursday, September 19, 2013

SONKOAWATUNUKU TIMU YA WANAWAKE YA MCHEZO WA VOLLLEYBALL.


Gideon Mbuvi a.k.a  Sonko,akiisaini  hundi hiyo


Senator wa jiji la  Nairobinchini Kenya  Gideon Mbuvi a.k.a  Sonko jana aliitunuku timu ya wanawake ya mchezo wa volleyball kiasi cha shilingi 300,000   kwa fedha za Kenya kwa kujituma na akawaahidi kuwaongezea kiasi kama hicho, endapo watafanikiwa kuwafunga timu kutoka Tunisia leo  .

Jana timu hiyo ya Kenya walifanikiwa kuwafunga timu kutoka Cameroon ukiwa ni ushindi wao wa awali kwa ushindi wa t 3-0 na hivyo kuendelea kushikilia record yao ya kutofungwa mpaka sasa katika michuano inayoendelea ya mataifa ya Africa na hivyo kujongea katika fainali za michezo hiyo kadiri siku zinavyo songa mbele katika kituo cha kimataifa cha michezo huko Moi vilivyoko katika  eneo maarufu la  Kasarani.

Mida ya saa kumi na moja jioni  hii inatarajiwa timu hiyo ya wanawake ya Kenya endapo itaishinda timu kutoka  Tunisia! Basi timu itatawazwa kuwa mabingwa katika nchi za kiafrica.

Sonko wakati akimkabidhi team manager Ednah Rotich hundi ya fedha hizo 300,000, Senator Sonko aliwashukuru wachezaji wa mchezo wa volleyball kwa kujitoa naye akawahakikishia kuwa ataendelea kuwaunga mkono wakanapoiletea sifa nchi yao kupitia kujituma na kujitoa kwa taifa.

Sonko pia aliahidi kupeleka sifa ya timu hiyo kwa viongozi wengine nchini humo na kwenda mbele zaidi kwa makamu wa rais hadi kwa rais Uhuru Kenyatta.

Kenyaimeshashinda michezo yote mine iliyocheza katika kombe la mataifa ya Africa iliyopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika uwanja wa  Kasarani ambapo nchi zilizoshiriki ni  : Kenya yenyewe , Egypt, Algeria, Cameroon, Senegal na  Tunisia itakayo kipiga leo.

No comments:

Post a Comment