
Lambert
Mende Msemaji wa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Serikali ya Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo imesema majeshi yake kwa kushirikiana na kile kikosi
maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi wa M23
kimewapiga waasi hao katika ngome yao ya mwisho.
Msemaji wa Serikali
Lambert Mende ameiambia BBC kuwa wapigani waliobaki wa M23 wanaweza wakawa
wamekimbia , wamevuka mpaka au wamejisalimisha.
Mende amesema kikosi
maalum cha majeshi ya nchi hiyo kimeharibu silaha za waasi hao usiku kucha na
inasadikiwa kiongozi wa kijeshi wa kundi hilo la M23 Sultani Makenga ni
miongoni mwa waliovuka mpaka na kuingia Rwanda au Uganda.
Wakati huo huo viongozi
wa nchi za SADC wanaokutana nchini Afrika Kusini wamezunguzia mgogoro wa
Jumuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwataka viongozi kundi la waasi wa M23
kutangaza kusimamisha mapigano.
Taarifa iliyotolewa
baada ya mkutano huo imesema kama waasi hao watachukua hatua hiyo mkataba wa
amani unaweza kusainiwa ndani siku tano zijazo.
No comments:
Post a Comment