
Ndugu Wahariri,
Salamu kutoka
HakiElimu,
Kufuatia tamko la serikali kuhusu upangaji wa viwango vya
alama, matumizi ya alama endelevu za mwanafunzi na ufaulu kwa kidato cha nne na
cha sita, HakiElimu imekuwa ikipokea maombi mengi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari kutaka kujua msimamo wa shirika kuhusu jambo hili kama wadau wakubwa wa masuala ya elimu.
Tafadhali pokea tamko rasmi kutoka HakiElimu kuhusu
msimamo wa shirika. Kimsingi uamuzi huu wa serikali umemshtua kila mtanzania na wengi wanajiuliza
tunatengeneza kizazi cha namna gani, hasa katika ulimwengu huu wenye ushindani
mkubwa sio tu kwenye soko la ajira; lakini pia maendeleo ya sayansi na tekinologia
ambayo pamoja na mambo mengi yanapelekea uhitaji mkubwa wa wataalamu waliobobea
kwenye masuala mbalimbali.
Tunaomba tushirkiane kwa pamoja kama watanzania wenye nia
ya kuona watoto wetu wakipata elimu bora na si kufaulu tuu mitihani. Mnaweza
kutumia tamko hili kwenye magazeti yenu kwa namna mtakavyoona inafaa.
Tunaamini kuwa mtatumia fursa mlizonzao kuelimisha umma
wa watanzania kuhusu jambo hili kuwa si la kufurahia kwa kile wazazi wengi
wanachodhani kuwa watoto wao watafaulu mtihani; bali kufikiria zaidi kuhusu
ujuzi na maarifa waliyopata kwa kipindi walichokuwa darasani na namna wahitimu
hawa watakavyoweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika ulimwengu wa sasa.
Asanteni sana kwa ushirikiano.
Benedicta Mrema | Media and Advocacy Email:
benedicta.mrema@hakielimu.orgMobile Phone: +255 713 068991; Office: +255 22
2151852/3; Fax: +255 22 2152449
Web: www.hakielimu.orgAddress: 739 Mathuradas Street,
P.O.Box 79401, Dar es salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment