Muoneano wa kichwa cha treni ambacho kinaundwa Upya na Kampuni ya SMH/Rail kutoka nchini Malaysia kikiendelea kufanyiwa kazi katika karakana ya Reli mkoani Morogoro. Kichwa hicho ni moja ya vichwa ambavyo vinajengwa upya kwa ajili ya kuimarisha usafiri wa Reli Nchini. Aidha, Kichwa cha kwanza kitakabidhiwa kwa Serikali Mwanzoni mwa mwezi Disemba 2013.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akioyeshwa mpango kazi wa kampuni ya SMH/Rail na Mhandisi wa Kampuni hiyo, Eng. Mohd Hisham(Kulia kwa Naibu Waziri) ambayo inaunda upya vichwa vya treni katika karakana ya Reli Mkoani Morogoro. Naibu Waziri ametembelea karakana hiyo leo Asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni ambavyo viko kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa kwenye sekta ya Uchukuzi.
No comments:
Post a Comment