

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan naye alikuwepo hapo uwanjani.



Mazungumzo ya hapa na pale






Viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika mashariki Jumatano Novemba 28, 2012 wamefungua rasmi wa barabara ya
Arusha – Namanga kwa upande wa Tanzania, na Namanga– Athi River kwa upande wa
Kenya, kama sehemu ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi unaofanyika Nairobi,
Kenya.
Barabara ya Arusha –
Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania
ilikuwa ni mojawapo ya shughuli za uzinduzi rasmi wa Makao Makuu Mapya za
Jumuiya uliofanyika mapema siku hiyo hiyo jijini Arusha, kabla ya viongozi hao
kuelekea Athi River kwa ufunguzi wa barabara hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Tanga–Horohoro, yenye
urefu wa kilomita 66 pia nao umekamilika na tayari imeanza kurahishisha
usafiri na usafirishaji baina ya Tanzania na Kenya na nchi nyingine wanachama.
Barabara nyingine zilizopo katika mtandao wa
barabara wa Jumuiya zinazoendelea kujengwa kwa upande wa Tanzania, ni pamoja na
zile za mtandao wa Dar es Salaam-Isaka-Lusahunga na Mutukula hadi Masaka;
Lusahunga-Nyakasanza hadi Rusumo, na Rusumo-Kigali hadi Gisenyi.
Nyingine ni Biharamulo - Mwanza - Musoma -
Sirari - Lodwar – Lokichogio; Tunduma - Sumbawanga - Kigoma - Manyovu (Mugina)
- Rumonge - Bujumbura - Ruhwa (Bugarama) – Karongi hadi Gisenyi, pamoja na ile
ya Tunduma - Iringa – Dodoma - Arusha - Namanga hadi Moyale.
Ujenzi wa barabara hizi utarahisisha usafiri
na usafirishaji wa bidhaa na huduma baina ya nchi wanachama, na hivyo kupunguza
gharama za uzalishaji na vilevile gharama za kufanya biashara katika nchi za
Jumuiya na hivyo kuvutia uwekezaji.
No comments:
Post a Comment