Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye suti nyeusi), akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Miundombinu wa namna usafiri wa treni Dar es Salaam unavyofanya kazi, katika kituo cha Stesheni ya Dar es Salaam jana asubuhi . Kamati ya Miundombinu imetembelea usafiri wa treni ya Dar es Salaam ya Shirika la Reli Tanzania (TRL
) kujionea namna usafiri huo unavyofanya kazi.
Mhandisi Richard Lauwo, akitoa ufafanuzi wa sehemu za kupandia treni(Platform) zilivyojengwa na Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli( RAHCO) kwa Mwenyekiti ya Kamati ya Miundombinu, Mhe. Peter Serukamba(Mb), katika stesheni ya Ubungo Maziwa.
Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu, Mhe. Peter Serukamba (Mb) akishuka kwenye Stesheni ya Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara iliyoifanya na wajumbe wa kamati hiyo
No comments:
Post a Comment