Mpigapicha na Mhazini wa Cha
Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) , LEAH SAMIKE anawatangazia kifo cha mume
wake Bwana HUMPHREY GEORGE LUPENZA aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Lucky
Construction Limited, (pichani) kilichotokea leo Saa 10: 55 alfajiri
katika Hospitali ya Hindu Mandal Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu
tokea Jumapili.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa
Marehemu, Kipunguni B -Ukonga Moshi Bar.Jirani na Kanisa la Pentekoste (Kanisa
la Mabati).
Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzako.
Marehemu ameacha Mke Leah William Samike na watoto 5 ambao ni Maximillian-Samike, Mary -Maria Clara, George, Harrison na Jane-Fatuma. Tuungane na familia ya Marehemu katika kuipa faraja

Humphrey akiwa na Mkewe Leah
Samike siku ya harusi yao mara baada ya kula kiapo chao cha ndoa cha kuishi
pamoja milele hadi kifo kitakapowatenganisha.
MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMINA.
No comments:
Post a Comment