Mwanamuziki Muhidini
Maalim Gurumo akiwa mahututi katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
MWANAMUZI nguli wa
muziki wa dansi nchini, Muhidini Maalim Gurumo aliyefahamika pia kama kamanda
na mashabiki wa muziki wa dansi, aliyeaga dunia Jumapili iliyopita katika
Hospitali ya Muhimbili jijini Dar, alikutana na mateso ya kwa saa 72 za mwisho
wake baada ya kulazwa akiwa taabani kwa siku tatu.
Mtoto wa marehemu
anayejulikana kwa jina la Abdalah aliliambia gazeti hili kuwa siku mauti
yalipomfika baba yake katika wodi namba sita Jengo la Mwaisela, alimtembelea na
kumkuta akiwa katika hali nzuri na alipopewa chakula alikula, akashiba lakini
cha ajabu alisema hatakula tena.
Kijana huyo alisema
muda mfupi baadaye, hali ya baba yake ilibadilika, akaanza kupumua kwa shida
ndipo alipozidiwa na baadaye kukata roho.
Maalim Gurumo akiwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kufikwa na mauti.Mzee Gurumo alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kwa muda mrefu na aliwahi kulazwa katika
hospitali hiyo ya Muhimbili.
Baadhi ya watu
waliomtembelea mzee Gurumo kwa nyakati tofauti akiwa hospitalini hapo ni pamoja
na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye
alimuombea afya njema na akaruhusiwa kurudi nyumbani.
Mzee Gurumo akiimba
wakati wa uhai wake.
Kifo chake kimeacha
simanzi si tu kwa familia yake, bali kwa wadau wa muziki wa dansi kwani alikuwa
mwalimu na kiongozi wa wanamuziki wengi ambao sasa wanatamba. Baada ya kustaafu
muziki, Mzee aliwahi kupewa zawadi ya gari na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb
Abdul ‘Diamond Platnumz’ aina ya Toyota Funcargo.
Akizungumzia msiba huo,
Kiongozi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki alisema wamempoteza mwalimu wa
muziki asiyekuwa na choyo ya kuelimisha.
Mzee Gurumo akiwa na
mkewe.
“Ni kama tumepoteza
tochi tukiwa kwenye msitu mnene usiku wa manane,” alisema.Naye msemaji wa Bendi
ya Mlimani Park Ochestra (Sikinde Ngoma ya Ukae), Jimmy Chika alipozungumza na
gazeti hili alisema mzee Gurumo aliwahi kuja kuwatembelea na kuimba mwezi mmoja
uliopita katika Ukumbi wa DDC, Kariakoo jijini Dar.
“Alikuja kama mara tatu
hivi ukumbini, naona alikuwa kama anatuaga kwa sababu alikuwa mwanzilishi wa
bendi na mbunifu wa mtindo wa Sikinde, aliubuni Septemba, 1978,” alisema
Chika.Mzee Kassim Mapili, mwanamuziki wa mkongwe, kwa upande wake alisema kifo
cha Gurumo ni pengo kubwa ambalo haliwezi kuzibika na akafafanua kuwa ni mtu
ambaye hakuwa mbinafsi.
Mzee Gurumo akiwa na CD yenye nyimbo zake cd ya mwisho kabla ya kifo chake.
Baadhi ya wanamuziki ambao amefanya nao kazi kwa karibu ambao sasa watakuwa wanamlilia mwalimu wao ni pamoja na Hassan Rehani Bitchuka, Said Mabela, Roman Mng’ande ‘Romario’ na wengine wengi.
Gurumo pia ameacha simanzi katika miji mbalimbali nchini kwa kuwa amewahi kutembelea kimuziki na alifanikiwa kujizolea mashabiki lukuki.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni msiba ulikuwa nyumbani kwake Mabibo, Dar huku taratibu za mazishi zikifanyika. Ameacha mjane na watoto wanne.
Mungu ailaze roho ya marehemu maali pema peponi. Amina.
Baadhi ya wanamuziki ambao amefanya nao kazi kwa karibu ambao sasa watakuwa wanamlilia mwalimu wao ni pamoja na Hassan Rehani Bitchuka, Said Mabela, Roman Mng’ande ‘Romario’ na wengine wengi.
Gurumo pia ameacha simanzi katika miji mbalimbali nchini kwa kuwa amewahi kutembelea kimuziki na alifanikiwa kujizolea mashabiki lukuki.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni msiba ulikuwa nyumbani kwake Mabibo, Dar huku taratibu za mazishi zikifanyika. Ameacha mjane na watoto wanne.
Mungu ailaze roho ya marehemu maali pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment