Tawi la mti wa mwarobaini.
Wengi wetu watasema wanaujua lakini hawajui maana ya
kuitwa muarobaini mti huo kwa kuwa mti huu ulipandwa nchini kwa amri ya kila
nyumba kuwa na miti hii japo miwili huku wenye maeneo ya biashara wakihimizwa
kuupanda mti huu kwa masharti kuwa asiyepanda basi atanyang’anywa leseni!
Si maneno ya mtu mwingine bali Kanali Yusuph Makamba
ambaye aliwahi kuwa mkuu wa mkoa huu wa Dar Es Salaam enzi hizo za mwanajeshi
huyu alipopata wazo la kuleta mbegu hii toka nchini India na kuupandikiza
kijeshi-jeshi maana anatujua fika watanzania kwa ubishi usio na maana hata kwa
maslahi yetu wenyewe.
Leo hii hasa vipindi hivi vya jua kali utakuta watu wote
wapo chini ya muarobaini wakipata oksijeni nyiiingi tu toka kwenye mti huo
jeuri bila kumbukumbu kuwa ulipandwa kwa viboko! Lakini, Angalau dozi ya
malaria sasa inagusa mitaa ya shilingi elfu kumi na zaidi huku watanzania bado
wanashindwa kutegua kitendawili cha mwanajeshi huyu mstaafu. Yeye amemaliza
kazi: Alikoutoa huo mti nchini India, unaitwa village Pharmacy na mlipomuuliza
huu ni mti gani aliwajibu kuwa huu ni muarobaini na alijua mtalishika hili jina
hadi mtakaposhindwa kumudu gharama za mahospitalini basi kila mtu atajua
mwarobaini ni nini kwa kuwa utatibu maradhi yote yatakayotusumbua watanzania na
kutunusuru na gharama hizi kubwa za madawa ya kemikali mahospitalini.
Nasikitika kuwa inawezekana siku tutakapolijua hili pengine mtaalamu huyu toka
jeshi la Tanzania anaweza akawa kaburini na tukabaki na historia yetu ya
kutangaza wema wa mtu baada ya kifo chake…
• Muarobaini
ukikamuliwa juisi yake umethibitishwa na vyuo vikuu vya tiba duniani
kuwa una uwezo wa kukinga maambukizi ya HIV nap engine kutibu kabisa ugonjwa wa
UKIMWI ambao husababishwa na virusi vya HIV.
•Muarobaini una uwezo mkubwa wa kuzuia aleji na kutibu
pia aleji za aina tofauti kama juisi yake itapakwa mwilini na hata kama
utainywa pia.
•Muarobaini huko Marekani na India umeonyesha uwezo
mkubwa wa kuzuia nyani dume kutoa mbegu za uzazi kwa majike na kugundulika kuwa
juisi ya muarobaini inamfaa mwanaume anayetaka kupanga uzazi bila kwenda
hospitali kwa vipimo, ushauri na kufanyiwa upasuaji mdogo kukinga uzalishaji wa
mimba (Vasectomy)
• Muarobaini pia ni kiboko kwa wanawake wasio na mpango
wa kushika mimba vilevile. Muarobaini kama utakamuliwa juisi yake na kupakwa
kwenye via vya uzazi vya mwanamke , basi juisi hiyo itamsaidia mwanamke kutopata
mimba zisizotarajiwa.
•Muarobaini una
uwezo mkubwa wa kupambana na kansa na hata kinga ya mwili pia. Tindikali
ziitwazo Polysaccharides na limonoids zilizomo katika magamba, majani na mizizi
huboresha kinga ya mwili haraka mno ili kupambana na maradhi kama kansa na
mengineyo bila uharibifu wa mwili kama zilivyo dawa kemikali za mahospitalini.
• Muarobaini hutibu kisukari kwa haraka sana. Majani
matatu tu ya muarobaini ni dozi tosha kwa mgonjwa wa kisukari na akizidisha
zaidi ya matatu basi anaweza kurudi hospitali na kuwaomba tena waganga
waitafute sukari kwenye damu yake kwa tochi! Maana muarobaini utaikomba sukari
yote kwenye damu hivyo usijiongezee dozi kijinga.
•Muarobaini hushambulia wadudu wote wanaoshambulia ngozi
ya binadamu kwa usahihi kabisa. Muarobaini hutibu mapunye, mba, ukurutu, upele
na magonjwa kadhaa ya ngozi bila madhara yoyote.
•Muarobaini hutibu magonjwa ya moyo. Huifanya damu kuwa
nyepesi itembee kwa mwendo sahihi na kuyafanya mapigo ya moyo kuwa tulivu kwa
wenye maradhi ya moyo.
• Mafua. Ujerumani ambako ni nchi ya baridi kwa kipindi
kirefu cha majira ya mwaka watu hufa kwa mafua tu! Tafiti walizofanya zinasema
juisi ya muarobaini hukata mafua haraka zaidi ya dawa yoyote ya hospitalini
huku ikikuhakikishia usalama bila madhara.
•Muarobaini unaua fangasi. Inawezekana una fangasi
miguuni, kwenye maungio ya siri kama mapajani, kwapani, sehemu za siri n.k.
tumia juisi ya muarobaini ujipake sehemu zilizoathirika kupambana na fangasi
hao bila madhara.
• Muarobaini pia ni dawa ya kufukuza wadudu bila madhara
ya kemikali. Jaribu kulala chini ya muarobaini lakini angalia pawe na majani
yake hapo chini halafu utaona hakuna usumbufu wa mbu wala nzi maana mwarobaini
hufukuza wadudu aina kadhaa akiwemo mbu!
•Wakala wa kulinda mazingira Marekani imeupitisha
muarobaini kama kinga bora ya kuhifadhia mazao dhidi ya wadudu waharibifu huku
ikidaiwa kwamba muarobaini hauna sumu mara 200 zaidi ya madawa ya kemikali na
mazao yanakuwa salama kwa matumizi ya binadamu,ndege na wanyama kwa ujumla.
Muarobaini pia hutibu malaria. Mchanganyiko maalum wa
majani ya muarobaini uitwao kwa kitaalam “irodin A” ni sumu ya kuzuia na kutibu
malaria. Majaribio mengi yamefanyika hata hapa nchini na muarobaini umeonekana
una nguvu ya kupambana na malaria hata hapa nchini Tanzania japo si mti wenye
asili yetu.
Nilipoingia katika tiba asili, wataalamu wengi
waliniambia kama nataka mafanikio ya haraka basi nianze na kutibu wagonjwa kwa
muarobaini. Naapa kwa watanzania wote kuwa nilifanikiwa sana maana hakuna
aliyerudi akasema hakupona ugonjwa wowote hivyo nina imani siku mwarobaini
ukitumika kama India basi utaitwa National Pharmacy….Na nina wasiwasi kuwa kama
wadau wa afya wakichelewa kuwajulisha wenye nchi taarifa hii muhimu tena kwa
vituo basi watakapogundua hili, matabibu wengi watakosa ajira maana hakuna
atakayeenda tena hospitali: akatafute nini?
Maana hata urafiki kati ya matabibu
na wenye nchi utapungua kwa kuwa watagundua kuwa walifichwa habari hizi ili
wawe mitaji ya wadau wa afya ambao ni sisi! Binafsi nimeanzisha kozi ya
kutengeneza vidonge vya muarobaini inayogharimu shilingi elfu sitini tu kwa
wenye familia zenye msimamo na tiba asili ili kesho niweze kujitetea kuwa
nilijitahidi kwa uwezo wangu kusambaza taarifa hizi kwa vitendo. Je, wewe mdau
wa tiba mwenzangu umechukua hatua gani? Nipigie tukutane ofisini siku ya
jumatatu, jumatano na Ijumaa pale machinga Complex Ilala Dar Es Salaam
tuyaongee kwa vituo. Ada ya mazungumzo ni shilingi elfu tano tu!
Asanteni kwa kunisoma na tuuenzi Muarobaini….
Tabibu John Haule
Machinga Complex, Kawawa road.
Room no. 35F, 36F and 37F
Kariakoo Dar Es Salaam
No comments:
Post a Comment