Monday, June 3, 2013

MKWAWA EVENT

Eneo la mbele la shule/chuo cha mkwawa
 
Shughuli yenyewe itakua  ni ijumaa ya tarehe 5 July, 2013, katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mjini opposite na chuo cha IFM, some key people waliosoma Mkwawa ni pamoja na Mh.Prof. Kahigi (Mb), Mh. Nyabari Nyangwine (Mb), Prof. John Nkoma, Prof. Mulokozi, Dr. Pindi Chana (Mb), Mzee Mwaokola Majogo, Dr. Luande (Ocean Rd. Hosp), Dr. Awiki, Dr. Magesa, Jaji Mkwawa, Mh. Mungai (Mb).....na wengine .
Sare ndo zilikua hivyo na hapo wanafunzi wako kwenye parade

Event hii inahusisha wale wooote waliosoma Mkwawa Sekondari tangu mwaka 1945-2005 kabla hakijawa chuo. Mchango wa event hii kwa kila kichwa ni Tsh. 50,000/- ambazo zitatumika kugharamia matangazo katika vyombo vya habari, vinywaji, chakula, ulinzi, mapambo, kukodi viti na meza, MC na muziki, live band na pia tutakichangia chuo cha Mkwawa kiasi fulani cha fedha ili kukarabati baadhi ya majengo ya chuo.
NA HIZI NI BAADHI YA PICHA ZA MUONEKANO WA SHULE/CHUO
 
Ua hapo unalifahamu ya zamaniii, mahafali hayo, pamepambwa nakwambia
Ngao ya shule/chuo cha Mkwawa
Muonekano wa shule/chuo cha Mkwawa
Wakati huoooo msosi tyme.
Bara bara hii ni ya lami itakayo kuongoza kuelekea Mkwawa school/chuo
hii itakupeleka shuleni/chuoni Mkwawa
Seth Benjamini, hii iko ndani.

1 comment: