Maharusi Bwana na Bibi Paul James wakiwa na wapambe wao ndani ukumbi wa
Shekinah Garden uliopo Mbezi Makonde wakisubiri kupokea zawadi kutoka kwa
wageni waalikwa mara baada ya kumeremeta mwisho mwa Juma kwenye Kanisa la St.
Gaspar Catholic la Kunduchi jijini Dar es Salaam
Mtangazaji wa Power Breakfast ya Clouds Fm Paul James a.k.a PJ afunga ndoa na Beatrice Wilbard Uiso.
Mtangazaji wa Power Breakfast ya Clouds Fm Paul James a.k.a PJ afunga ndoa na Beatrice Wilbard Uiso.
Bwana na Bibi Paul James katika pozi matata ndani ya ukimbi wa
Shekinah Garden uliopo Mbezi Makonde mara baada ya kumeremeta katika kanisa la
St. Gaspar Roman Catholic lililopo Kunduchi jijini Dar.
Pichani juu na chini ni
wageni waalikwa wakitoa mkono wa pongezi kwa maharusi.
Mrs. Paul James akiserebuka na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa mnuso
wao wa nguvu uliokuwa ngumzo katika jijini la Dar es Salaam
Picha juu na chini ni
wageni waalikwa, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria harusi ya Bwana na Bibi
Paul James mwishoni mwa juma ndani kiota chenye hewa safi cha Shekinah Garden
kilichopo Mbezi Beach.
Wadau wakibadilishana
mawazo hapa na pale.
Mdau Isack Muyenjwa Gamba
wa Radio One (kushoto) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa huku wakitoa tabasamu
bashasha mbele ya camera yetu.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa
Clouds Radio Gerald Hando wakati wa mnuso wa Harusi ya PJ.
Baba mzazi wa PJ
akimkabidhi mwanae zawadi ya kimila Upinde na Ngao kama ishara ya kuilinda
ndoa.
Bwana harusi PJ akionyesha
zawadi yake kwa wageni waalikwa.
Kiongozi wa kikundi cha
Umoja cha Kunduchi wakikabidhi zawadi yao kwa Maharusi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akiongoza wafanyakazi wa kampuni yake
kutoa mkono wa pongezi kwa maharusi. Kampuni ya Montage ilihusika kupendezesha
ukumbi huu pamoja na kuandaa Cake ya Maharusi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda na wafanyakazi wa kampuni yake wakitoa
mkono wa pongezi kwa maharus
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akikabidhi zawadi ya Fungate (Honey Moon)
kwa maharusi iliyotolewa na Serena Hotel kwa kushirkiana na kampuni yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda na wafanyakazi wake katika picha ya pamoja
na maharusi.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda na wafanyakazi wake wakirudi kwenye siti
zao.
Wafanyakazi wa Clouds
Media Group wakiongozwa na Sebastian Maganga (suti ya kijivu) kwenda kutoa
mkono wa pongeza kwa mfanyakazi mwenzao.
Clouds Media Group ikitoa
mkono wa pongezi kwa maharusi.
Sebastian Maganga
akitangaza zawadi kwa niaba ya Kampuni ya Clouds Media Group.
Vicheko, nderemo na vifijo
vilitawala ukumbini hapo..Kushoto ni MC wa Shughuli Regina Mwalekwa na Barbara Hassan
(mwenye gauni jeusi) akiwa mwenye furaha kuona mtangazaji mwezie wa kipindi cha
Power breakfast kapata jiko.
Power Breakfast ya Clouds
Fm nayo haikubaki nyuma ilitoa voucher za Shopping kwa maharusi..... Mtangazaji
wa kipindi cha Power Breakfast Gerald Hando akitangaza zawadi yao mfanyakazi
mwenzao.
Na hii ndio kamati ya
maadalizi iliyofanikisha mnuso huo wa nguvu uliofanyika mwishoni mwa juma ndani
ya Shekina Garden iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Maharusi Bwana na Bibi Paul James wakifungua muziki. Camera yetu
iliishia hapo kama kuna picha za ziada basi tutawamuvuzishia
Kwenye Upande wa Video na
Still Pictures ilihusika kampuni ya Ongea na Janet inayomilikiwa na Janet
Sosthenes Mwenda ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Ongea na Janet.
Pichani mwanadada huyo akiwa busy katika kuchanganya picha kwenye mnuso huo.
No comments:
Post a Comment