Friday, June 14, 2013

MSANII WA HIP HOP LANGA AFARIKI DUNIA



LANGA

Langa alishiriki shindano la Pop Star akiwa na wenzake wengine wawili Sara Kaisi 'Shaa' na Witness Mwaijaga 'Witness' na waliunda kundi lilioenda kwa jina la Wakilisha.

Wakiwa na kundi la Wakilisha Marehemu Langa na Wenzake hao walitamba sana kwa nyimbio mbili za 'Unaniacha Hoi' na 'Kiswanglish'.

Langa aliamua kutoka kivyake na kuachia kibao chake cha kwanza cha 'Matawi ya Juu' na video ya wimbo huo ikaingizwa katika mashindano ya MTV Base na baade kushinda tuzo ya Kisima nchini Kenya.

Aliwahi fanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini na nje ya nchi kama vile kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin Wyre).
Maisha ya Langa kimuziki yalianza kuporomoka pale alipoachia albam yake ya 'Langa' na kushindwa kuuza baada ya kukataliwa na wasambazaji na akaamua kutumia dawa za kulevya.
Baada ya jitihada za familia yake aliweza kuondoka katika maisha hayo ya uteja na alipo toka aliachia nyimbo za 'Bombokiata' na 'Mteja Aliyepata Nafuu'.
Langa alizaliwa mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Msingi Olympio na baade  Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.


Akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda.
Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.

Buriani Langa.

No comments:

Post a Comment