Thursday, November 29, 2012

MUENDELEZO WA PICHA ZA MAZIKO YA SHARO MILLIONEA


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole  Zaina Mkieli, Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
. Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nauye pamoja na Waziri Njenje, wakitupa mchanga kaburini.
Waombolezaji wakimsaidia mwenzao aliyepoteza fahamu msibani, wakati wa mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu Tanzania, yaliyofanyika, kijijini kwa marehemu, Lusanga, Muheza mkoani  Tanga.
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu Tanzania, Hussein Ramadhani, maarufu Saharo Milionea, likiswaliwa  nyumbani kwao, Lusanga, Muheza mkoani Tanga
Mzee King  Majuto akitupa mchanga kaburini kumzika Sharo Milionea.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Rais wa Bongo Movies Simon Mwakifyamba na Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea.
Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva, wakati wa mazishi hayo.
Baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva na filam Tanzania, wakiwa kwenye mazishi ya Sharo milionea.
.Mkuu wa wilaya ya Muheza, Subra Mgalu akisoma salam za Shirika la Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) la Mama  Anna Mkapa, kwenye msiba huo. Pamoja naye ni Nape na Simon Mwakifamba.
. Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando  aliyefunga mikono na amevaa shati nyeusi na ufito mweupe akiwa na  baadhi ya wasanii kwenye mazishi hayo.


Vijana wakiwa wamepanda  mnazi kuona mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga.

No comments:

Post a Comment