Tuesday, November 27, 2012
MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI NAIROBI, KENYA
Mwanasheria wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiongoza Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo. Kushoto ni bwana Wilbert Kawa Katikati ni bwana Dr. Richard Sezibera na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano Uganda. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Kenyetta jijini Nairobi
Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samweli Sitta pamoja na Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyemba (wa pili kulia) , Waziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika (kushoto) na Mhe Ole Nangoro Naibu Waziri Kilimo na Mifugo (kulia) wakifuatilia kwa makini jambo katika Mkutano wa Baraza la Mwawaziri wa Jumuiya Jijini Nairobi.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda (kulia) akifuatilia kwa makini mkutano unaoendelea Nairobi katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment