Tume moja ya serikali ya Zanzibar imependekeza kushtakiwa kwa mmiliki wa meli na maafisa wote wa bandari waliohusika na ajali ya boti mwezi Julai iliyopoteza maisha ya watu 81 na kusababisha zaidi ya 200 ambao bado hawajapatikana, liliripoti gazeti la Daily News .
"Mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti yanajumuisha hatua za kisheria na kinidhamu dhidi ya wale wote waliotajwa ndani yake," alisema Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar na kiongozi wa tume hiyo, Abdulhakim Ameir Issa. "Tume pia imeishauri serikali kupitia sheria za usalama baharini na kuimarisha idara ya uokozi na udhibiti wa majanga."
Ripoti ya tume hiyo ilitaja uzembe, ufanyaji kazi usio wa kitaalamu na kutowajibika kama sababu kuu za ajali ya meli ya MV Star Gates, ambayo ilikuwa ya pili kuzama ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. Tume hiyo pia ilithibitisha kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba abiria 447, zaidi kabisa na idadi ya abiria 290 iliyotajwa katika orodha rasmi ya abiria.
Ripoti hiyo pia ilitaka kufidiwa kwa kila mtu aliyehusika kwenye ajali hiyo, zikiwemo familia za marehemu, wale waliojeruhiwa na wasiojeruhiwa kwa angalau shilingi 125,000 (dola 78) kila mwezi kwa miezi 80.
No comments:
Post a Comment