Monday, November 5, 2012

TANZANIA YAONGEZA MIUNDOMBINU!


           Sehemu ya barabara ya Minjingu-Babati-Singida iliyozinduliwa na Rais Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero wakifurahia baada ya kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John  Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akipanda mti kama kumbukumbu baada  ya  Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier  wakiweka  jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maeneo ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe  kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John  Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu

No comments:

Post a Comment