Thursday, November 15, 2012

SWAHILIWOOD YAWALETEA BORA ZA 2012



Tuzo za Bora za 2012 kwa mwaka huu.
BAADA ya miaka miwili kuwatunuku wasanii wetu BORA ZA 2010 kimya kilitawala tumeona mengi ambayo yanapaswa kupongezwa katika tasnia ya filamu, kuna mengi mazuri yanayofanywa na wadau wa tasnia ya filamu Swahiliwood, kupitia mtandao wako mahiri wa filamu Tanzania FC tunaonyesha kuwa tunawajali wadau wa tasnia ya filamu tunakuja na tuzo zinazojulikana kwa jina la BORA ZA 2012.

Kumekuwa hakuna utamaduni wa utoaji wa tuzo kila mwaka katika tasnia ya filamu jambo ambalo linadhorotesha ukuaji wa tasnia hiyo kwani watu wanakosa sehemu ya kujipima kuhusu ubora wa kazi zao, kukosakana kwa tuzo ndani ya tasnia ya filamu yenye miaka zaidi ya kumi na 13 ni aibu, tuzo hizi mara nyingi ukwamishwa na taasisi ambazo zaidi ya kukusanya fedha hawajawahi kuandaa.


Prof. Martin Mhando akimpata tuzo msanii chipukizi Jenifer mwaka 2010.
Hayati Kanumba akiwa na tuzo kibao kutoka FC Bora za 2012.
Pamoja na mikingamo isiyo na tija kutoka katika taasisi mbalimbali mtandao huu hauwezi kushindwa kuwatunuku wale wanaostahili kutunikiwa tuzo zao kulingana kazi zao kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeona, tumetambua uwepo wao na kazi zao pia, tunawaunga mkono kwa BORA ZA 2012.
Watayarishaji wa filamu ni wakati wenu wa kuwakilisha filamu zilizotoka mwaka 2012 na kuingia sokoni kwa ajili ya kupigiwa kura na wapenzi wenu wa filamu pia kwa wale wasanii chipukizi wakilisheni kazi zenu mlizoshiriki na kuingia sokoni kwa mwaka 2012.
Bora za 2012 zitawaleta washindi kwa utaratibu wa kupiga kura kupitia mtandao huu , kutuma ujumbe mfupi, wahusika ni wale wapenzi wa filamu Swahiliwood ambao utembelea katika mitandao mbalimbali na vyombo vya habari kwa ujumla, tutakuwa na vipengere 10.
.
Bora za 2012
MAKUNDI YA FILAMUCENTRAL BORA ZA 2012.
Msanii chipukizi wa mwaka
Muigizaji bora wa kike
Muigizaji bora wa kiume
Mwandishi bora wa Mswaada
Mchekeshaji Bora
Mtayarishaji bora wa filamu
Kampuni bora ya utengenezaji filamu
Msambazaji Bora
Muongozaji Bora
Tuzo Maalum

TEMBELEA FILAMU CENTRAL.CO.TZ

No comments:

Post a Comment