Rais
Jakaya Kikwete ameiasa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika (SADC)
kuimarisha ushirikiano kati yake na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili
kufanikisha utekelezaji wa Mkakati wa pili wa kushughulikia masuala ya Siasa,
Ulinzi na Usalama wa Jumuiya hiyo.
Amesema
ili malengo ya Mkakati huo yaweze kufanikiwa ni lazima ushirikiano wa ndani na
nje wa nchi hizo wanachama uimarishwe na kuongeza kuwa SADC haiwezi Kutegemea
mikakati ya ndani ya ulinzi na Usalama ya nchi fulani kutaka kutekeleza mkakati
wake.
"SADC
haitakiwi kuiingilia kwa kutaka kuibadili mikakati ya ndani ya Nchi wanachama
ya ulinzi na usalama badala yake washirikiane kwa karibu kuangalia nini cha
kufanya" .Kuhusu umuhimu wa mkakati huo Rais Kikwete amesema utakuwa
muongozo wa SADC katika masuala yote ya ulinzi, usalama na siasa, na umejikita
katika kutatua vikwazo mbalimbali vya kiulinzi vilivyopo.
Amefafanua kuwa Utekelezaji wa SIPO na maazimio yake utapelekea hali ya amani
na utawala bora kwa Nchi nyingi za Afrika na kuongeza kuwa katika awamu ya pili
ya SIPO mabadiliko mengi yamefanyika yakiwemo uongezaji wa vipaumbele katika
mfumo wa utekelezaji na ufuatiliaji wa masuala ya ulinzi na usalama.
Uzinduzi
wa SIPO II utaangalia ushirikiano kati ya Nchi wanachama, ushirikiano katika
masuala ya kibiashara, uhakika wa kushughulikia masuala ya upatikanaji wa Amani
na ushirikiano katika nyanja ya habari.
Akieleza
historia ya chombo cha Usalama cha SADC alisema kabla ya kuanzishwa kwa chombo
hicho kulikuwa na ushirikiano wa nchi katika masuala ya ulinzi na usalama na
kubainisha kuwa kuanzishwa kwa SIPO kunatokana na nchi wanachama kuona umuhimu
wa kuwa na chombo kinacho waongoza katika masuala hayo yote.
Awali
akizungumza na wajumbe wa mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Benard Membe amesema kuwa SIPO imekuwa ni nyenzo muhimu nay a
kutegemewa na nchi za SADC katika masuala yote ya usalama.
Amesema
SIPO ilizinduliwa rasmi mwaka 2004 na baadae kufanyiwa marekebisho ya kimsingi
mwaka 2007 na kueleza kuwa kutokana na marekebisho hayo ya Mwaka 2007
ilikubaliwa kuwa mikakati na vapaumbele vya SIPO iwe inapitiwa kila baada ya
miaka mitano.
Aidha
uzinduzi huo utafuatiwa na mafunzo mbalimbali yatakayoendeshwa na wataalamu kwa
muda wa siku nne.
No comments:
Post a Comment