Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, imetoa kibali
cha kukamatwa kwa mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Bi
Simone, Gbagbo. Bi
Gbagbo anasakwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kivita wakati wa vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilivyoibuka baada ya uchaguzi wa urais nchini humo.
Mumewe
tayari alishakamatwa na anasubiri kesi yake kuanza katika mahakama hiyo iliyoko
The Haque, kuhusiana na madai hayo ya uhalifu wa kivita.Takriban watu 3,000
waliuawa kwenye machafuko yaliyotokea baada ya ya Gbagbokukataa kukubali
matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Bi Simone alipoibuliwa handakini wakati wanakamatwa na mumewe wakati huo na kuwekwa chini ya ulinzi.
Na hapa wanajeshi waliomkamata Gbagbo wakiondoka naye.
Wanajeshi
wa rais wa sasa wakiungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa walianzisha
msako mkali dhidi yao, baada ya kujificha ndani ya ikulu ya rais.
Licha
ya kuwa Bi Gbagbo hakuwa akiwania kiti chochote cha kisiasa, ripoti zinasema
kuwa alikuwa na mamlaka makubwa na kuwa alimshawishi mumewe kutokubali matokeo ya uchaguzi.
Gbagbo,
67, alihamishwa hadi The Haque mwaka uliopita, na kuandikisha historia ya kuwa
rais anayeondoka wa kwanza kufikishwa mbele ya mahakama hiyo ya ICC.Rais huyo
wa zamani amekanusha madai hayo yote.
Kabla
ya kuhamishwa hadi the Haque, Gbagbo na mkewe mwenye umri wa miaka 63,
walifunguliwa mashtaka nchini Ivory Coast kuhusiana na uhalifu wa kiuchumi, ikiwemo
mdai ya kupora mali, wizi wa nguvu na kutumia rasilimali za umma kwa njia mbaya
Mahakama
hiyo ya ICC sasa imetoa wito kwa serikali ya Ivory Coast, kumusafirisha Bi
Gbagbo ili afunguliwe mashtaka huko the
Haque
No comments:
Post a Comment