BBC inasikitika kutangaza kifo cha mtangazaji Fred Mtoi ambaye alifariki Ijumaa usiku mjini London.
Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kwenda Ulaya kwa mafunzo.
Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.
Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.
Alishiriki pia katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.
Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi TanzaniaFrancois Bin Swedy Mwinyi Alipenda kutangaza tangu darasa la 4 kwa kushiriki mama na mwana RTD na baadaye kutangaza PRT ya RTD. Mola ampumzishe salama, Aamiin.
cecy Brown Nkonya Oh jamani rip our bro...so very sad
BWANA AMETO, BWANA AMETWAA ,JINA LA BWANA LIHIMIDIWE! PUMZIKA KWA AMANI KAKA FREDDY MTOI.
No comments:
Post a Comment