Majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC la
mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka 2012 yametangazwa.
Yaya
Toure, kwa mwaka wa pili mfululizo, yupo kwenye orodha hiyo.
Mwenzake
katika timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba pia yumo.
Wachezaji
wengine ni pamoja na Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na
nahodha wa timu ya Zambia, Christopher Katongo.Huu umekuwa ni mwaka wa ufanisi
kwa wachezaji hao, na timu za wachezaji wanne zikionyesha ustadi kwa kupata
vikombe.
Inaelekea
Drogba aliondoka Chelsea wakati muwafaka, mara tu baada ya timu yake
kukamilisha msimu kwa ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya, hii ikiwa ni mara
ya kwanza katika historia ya klabu, na vile vile akipata bao la ushindi katika
fainali ya Kombe la FA.
Raia
mwenzake wa Ivory Coast, Toure, naye akiichezea Manchester City, aliihakikishia
timu yake ubingwa wa ligi kuu ya Premier kwa mara ya kwanza; kombe lao muhimu
zaidi katika kipindi cha miaka 44.Belhanda aliisaidia timu yake ya Ufaransa ya
Montpellier kupata ushindi katika ligi ya Ufaransa daraja la kwanza, kwa
kufanikiwa kupata magoli 12 katika msimu.
Katika
mapambano ya kimataifa, Katongo, kutoka Zambia, naye akiiongoza timu kama
nahodha, alifanikiwa kuiwezesha timu yake ya Chipolopolo kuishinda Ivory Coast,
na kuibuka mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kuishinda Ivory
Coast katika fainali, kupitia mikwaju ya penalti.
Ba
hakung'ara katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya Senegal
kuondolewa katika hatua ya makundi, lakini binafsi aliweza kuifanyia timu yake
ya Newcastle kazi nzuri, na msimu uliopita alitangazwa kuwa mshambulizi bora
zaidi, kwa kufunga jumla ya magoli 17, na kuiwezesha timu kumaliza katika
nafasi ya tano
No comments:
Post a Comment