Brass Band
ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya
wanawake yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya
Afrika (WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam .
Washiriki wa Maandanamo ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake
yaliyoratibiwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika
(WILDAF),yaliyoanzia katika Viwanja vya Mnazi Mmoja na kumalizikia kwenye
Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.
Maandanamo
yakipokelewa na Muwakilishi wa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Mambo ya
Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Dora
Msechu (wa tatu kulia),Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na
Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula,Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema (pili kulia) pamoja na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kinondoni,Charles Kenyera.
Balozi wa
Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan akikata utepe uliokuwepo kwenye
basi aina ya Toyota Coster,ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Safari ya Wadau wa
Wildaf wanaokwenda Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea
kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali katika mikoa ya kanda hiyo kuhusiana
Ukatili dhidi ya Wanawake.
Wadau wa
Wildaf wakipanda kwenye Basi hilo tayari kwa Safari ya Mikoa ya Kanda ya
Kaskazini kwa ajili ya Kuendelea kutoa Mafunzo kwa Watu mbali mbali
katika mikoa ya Kanda hiyo kuhusiana Ukatili dhidi ya Wanawake.
Mwenyekiti
wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika
(WILDAF),Mh. Naomi Kaihula akisisitiza jambo wakati akitoa neno la
Ukaribisho katika Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo
"FUNGUKA - Kemea Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike"
uliofanyika mapema leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es
Salaam leo na kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.
Mwenyekiti
wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika
(WILDAF),Mh. Naomi Kaihula (pili kupia) akitoa neno la Ukaribisho katika
Mkutano wa Wadau wa Wildaf wenye kauli mbiu isemayo "FUNGUKA - Kemea
Ukatili Dhidi ya Wanawake !!,Sote Tuwajibike" uliofanyika mapema
leo,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam leo na
kuhudhuliwa na Wadau mbali mbali.Wengine Pichani toka kulia ni,Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Mkurugenzi wa Mambo
ya Ulaya na Amerika,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa,Balozi Dora Msechu,Mkugenzi Mkuu wa Shirika la Wanawake Katika
Sheria na Maendeleo ya Afrika (WILDAF),Judith Odunga pamoja na Balozi
wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan.
Muongozaji wa Mkutano huo,alikuwa ni Bw. Deus Kibamba
Kamishna
Msaidizi wa Jeshi la Polisi nchini,DCP Rashid Omar akiwasilisha mada ya
aina mpya ya Karatasi maalum itolewayo na Polisi iwapo mtu anapatwa na
tatizo la Majeraha (PF 3) iliyofanyiwa Marekebisho na kuongezewa baadhi
ya Vipengele Muhimu,wakati wa Mkutano uliofanyika leo wa Kupiga Vita
Ukatili dhidi ya Wanawake,kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es
Salaam.
Balozi wa Ireland nchini,Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) akizungumza machache kwenye Mkutano huo.
Mgeni
rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh.
Angella Kairuki akisoma Hotaba yake mbele ya Mamia ya Wadau wa Wildaf
waliohudhulia Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika Mkutano huo,ambaye ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh.
Angella Kairuki akikata Utepe wa Kuashiria Uzinduzi rasmi wa aina mpya
ya PF 3 mara baada ya kutoa Hotuba yake huku akisaidiana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema,Kushoto
ni Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya
Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Washiriki wa Mkutano huo wakisikiliza kwa Makini.
Makamanda wa Polisi wa Mikoa ya Kipolisi ya Dar es Salaam wakifuatilia Mkutano huo.
Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini,Inspekta Jenerali Said Mwema akiteta jambo
na Mwenyekiti wa Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya
Afrika (WILDAF),Mh. Naomi Kaihula.
Mrisho Mpoti na Mjomba Band wakitoa Burudani wakati wa Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment