Thursday, November 8, 2012

HUU NDO UANAMAPINDUZI COMRADE KIKWETE!


                
                              Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete  
     

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza furaha na shangwe yake kufuatia ushindi wa , Jumanne, Novemba 6, 2012 wa Rais Barack Obama wa Marekani katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.
Katika salamu zake za pongezi kwa kiongozi huyo wa Marekani ambaye amechaguliwa tena na wananchi wa nchi hiyo kwa kipindi cha pili, Rais Kikwete amesema mapema leo, Jumatano, Novemba 7, 2012:“Nimepokea kwa furaha na shangwe habari za kuchaguliwa tena kwako kuwa Rais wa Marekani kwa kipindi cha pili.
Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kukutumia wewe na kupitia kwako Chama cha Democratic pongezi nyingi kwa ushindi wako wa maana sana.”
Ameongeza Rais kikwete katika salamu zake hizo: “Kuchaguliwa kwako tena kuendelea kuongoza nchi yako muhimu na wananchi wake, ni ishara ya wazi ya uaminifu na imani ambayo wananchi wa Marekani wanayo katika uongozi wako wa mfano.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua tena uongozi wa nchi hiyo katika kipindi chako kipya, napenda kukuhakikishia msimamo wangu binafsi na ule wa Serikali yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa na wewe na Serikali yako ya kutukuka, ili kuendeleza uhusiano bora ulioko kati ya nchi zetu mbili ndugu.”
SALAM ZAENDELEA KUTOLEWA!





Nauthamini uhusiano wetu na tutazidi kuuimarisha baina yetu kwa miaka ijayo amesema rais Jackob Zuma,na kueleza kua Marekani ina mchago mkubwa sana katika maendeleo ya bara la Africa.
Na Kwa ushindi huu, Obama anakua ni Rais wa pili kutoka chama cha Democrat  kushinda awamu ya pili ya kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 4 katika ikulu ya nchini hiyo tangu kwisha kwa World War Two.

No comments:

Post a Comment