Wednesday, May 9, 2012

Ah MDALASINI Weeeee

Kutokana na kwamba pwani mie ndo kwetu! Hivyo viungo,desturi na baadhi ya tamaduni zinazofaa za pwani mie huniacha hoooi kwakweli bila kuficha moja ya viungo ninavyovipenda sana ni mdalasini! Napenda kuinywa yenyewe nikiwa nimeichanganya na asali, ama kuweka kwenye chai iwe ya vipande ama unga unga! Lakini mdalasini pia hupenda kuutumia kupika pilau la Zanzibar, kule unguja na pemba. Kama unanielewa basi napenda na viungo vyoooote vinavyowekwa vizima vizima katika pilau la pande hizo za Zanzibar.
                                                
                                                    huu ndo mti wa mdalasini,huwa mkubwa

                                     
                                                 hapa ukiwa umevunvwa tayari kwa matumizi



                              kijiti kina mambo hichoooo! asanteeeh
lakini nisiwe mchoyo bureee! mdalasini ni kama alivyo kinyonga, utumie utakavyo, wenyewe hauna hiyana unakubali tu! tuitazame  Custard ya mdalasini.

VIPIMO
Maziwa 2 1/2 Vikombe
Mdalasini wa unga 1 Kijiko cha chai
Mayai 3
Asali 1/4 Kikombe
Chumvi Kidogo (dash)
Vanilla 1 Kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1. Washa oveni moto wa 375F.
2. Weka vibakuli 6 maalum (remekins) vya kupikia kwenye oven , katika trei ya kuvumbika (bake).
3. Pasha moto maziwa, mdalasini na vanilla katika sufuria.
4. Chukuwa bakuli na uchanganye mayai, asali na chumvi pamoja.
5. Endelea kukoroga, huku unamimina ule mchanganyiko wa maziwa
kidogo kidogo hadi ichanganyikane vizuri.

6. Mimina custard kwenye vibakuli ulivyovitayarisha, kisha weka treya
kwenye mlango wa oveni na umimine maji ya moto (yaliyochemka) ili
itapakae chini ya vile vibakuli nusu yake.
7. Pika (bake) katika oven kwa muda wa dakika 30-40 au mpaka ukitovya kisu kitoke kisafi.

8. Ikisha iiva na kupoa, weka ndani ya friji na ikishapata ubaridi
itakuwa tayari kwa kuliwa.
WATAALAMU WA MASUALA YA KIMAHABA
 wanasema kuwa! Ukichukua asali vijiko 3, mdalasini vijiko 3 na tangawizi vijiko vya chakula 3 ukichanganya na maji glass 1 kisha ukaiacha kwa dk 15, halafu ukachuja na kunywa! Huongeza handasi, muda wa mechi huongezeka na uimara wa SEBAMASHIKU! LOL lakini pia  mchanganyo huo huongeza  joto mwilini na kuongeza raha ya game lol nimewahi kusikia tu mwayaaaaaa!
hakuna ziada mbovu! na hii ni kwa muujibu,wa
Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.
Hutibu ukungu wa miguuni - fangas
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha kwenye kipindi cha wiki moja

Maumivu ya jino
Changanya asali, maji kidogo  na mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka
Mdalasini  pia umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili kuongeza uwezo wa uzazi kwa kina mama wenye kuhitaji kuzaa.

Umri wa kuishi
Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vine{vikubwa} vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10. kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na kinywaji kingi.
jaribu na wewe leo uone tofauti,ni viungo ama tiba ya asili isiyo na madhara bali faida tupu.


1 comment:

  1. Dada umenipa darasa la kutosha leo hii hii naianza kazi. Jamani dawa tunazo hatuna utaalamu nazo tunaishia kwa Wachina, hawanipati tena. Ubarikiwe tuletee meengi hasa sie kina mama mwenzio tuimarishe nyumba zetu mwaya. Ni mimi mdogo wako Malaysia

    ReplyDelete