Monday, May 28, 2012

Lady Gaga avunja Onesho lake Baada ya Kupokea Vitisho


Lady akiongoza makamuzi kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards



Mwanadada mbunifu wa maonesho ya jukwaani Lady Gaga ameahirisha tour yake ya kimuziki Asia baada ya kutakiwa kufanya hivyo na watu wa usalama wa Indoneshia baada ya tishio kutoka kwa viongozi wakuu wa kiislamu nchini humo.
Nyota huyo wa miondoko ya pop alikua akiipigia promo  album yake ya born this way ball ,ilimpasa kuahirisha show yake baada ya kuelezwa ukweli kua akitia mguu wake katika jiji la Jarkata basi ajue watashughulika naye.
Chama cha kutetea uislam The Islamic Defenders Front (FPI) kilitoa msimamo wao juu ya mavazi ya Lady Gaga kua yana shawishi ngono na uchezaji wake vinaweza  kuwatia majaribuni vijana wa Indoneshia na waislamu walio wengi katika taifa lao.na wakatamka wazi kua Gaga akijitia kichwa ngumu basi watamdhuru na wakamwita wakala wa shetani ambae huvalia sidiria tupu na chu** tu.
Pamoja na matangazo kibao kufanywa lakini management ya Gaga  wanatazama kitisho hicho kwa jicho la tatu na kuita kua ni lengo la kushusha moto wa tamasha la june 3 atakalofanya Gaga , ndipo mwanasheriaMinola Sebayang  ambaye ni promoter wa Big Daddy Promotion alipomtaka Gaga kuahirisha tour hiyo na kusema kua hawatawasamehe walowatisha .
Chama hicho cha FPI kimeendelea kueleza kua Indoneshia italindwa na kuepushwa na dhambi zitakazo sababishwa na shetani huyo,japokua chama hicho chenye mrengo wa kiislam kutoa vitisho hivyo! Raia wa nchi hiyo tiketi zipatazo 50,000 zilisha uzwa na ilitegemewa kua ndo tour kubwa kuliko zote kuwahi kufanywa Asia.
Management ya Gaga imeshangazwa na wana usalama wa Indoneshia walipowataarifu kua kutokana na sababu za kiusalama Tour ya Gaga katika nchi yao haitowezekana,serikali ya nchi hiyo ilishaonesha ushirikiano ,lakini tishio hilo ni kubwa kuliko mtu kukosa kibali cha kuingia katika nchi hiyo.
Saa chache kabla ya tangazo hilo kutolewa,mwanamuziki Lady Gagag mwenye follower milioni 25 katika account yake ya twitter alitupia kauli hii "There is nothing Holy about hatred."
Mwenyekiti wa chama hicho cha FPI ambaye anadai ana followers milioni 7 kwenye akaunti yake ya twitter wamefurashishwa na uamuzi wa Lady Gaga kutokwenda nchini kwao, awali FPI  wamesha shambulia  clubs na pubs kibao  na wamewataka mashabiki wa Lady kuacha kulalama na wajirekebishe na kama haitoshi waache kumwabudu shetwan.
FPI wanaendelea kufunguka kuwa wao kama wao walisha nunua tiketi kama 150 hivi ili kupata nafasi ya kua sehemu ya washiriki ili wapate nafasi nzuri zaidi ya kusimamisha show hiyo endapo ingelazimu kufanywa.
Kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali na pia mwenye dhamana ya mahusiano ya kidini  waziri Suryadharma Ali amefurahiwa na vuguvugu hilo la kumsimamisha Gaga kwa kufanikiwa kufanya hivyo na akasherehekea kufanikiwa huko na kusema kuahirishwa kwa tour hiyo ni kwa manufaa ya nchi yao  na kueleza kua Indoneshia burudani haikataliwi mradi iwe ya kistaarabu  na si vinginevyo  no!
Pamoja na FPI kumtia mkwara Lady Gaga, kuna waliotangulia kufanya show nchini humo kama Beyonce na Pussycat Dolls wao walisoma alama za nyakati na kuvaa vyema ili tu wapaafom na walifanikiwa.
Pamoja na hayo yote Maelfu ya followers wa Gaga walimtumia tweet kibao wakimtaka Gaga asihofu chochote bali aendelee na mipango yake kama kawaida, kijana mwenye umri wa miaka 17 Agus Murdadi amesubiri kwa  miezi kadhaa kumuona Lady Gaga ,na akaeleza hisia zake kua ameshtushwa sana na taarifa kua Lady Gaga hata kwenda tena nchini mwao kwa mtazamo wake Lady ni mbunifu na sio mhamasishaji ngono.na kuahidi kumtumia tweet Lady kua asihofu aende tu nchini mwao na kusema polisi wanaweza kuwazui FPI wasifanye chotechote nay eye kwa nafsi yake anawachukia FPI.
Lady Gagag ana show zipatazo kama 3 hivi , huko Singapore wiki hii  kabla hajakwea pipa kuelekea New Zealand na Australia na baadae Ulaya kumalizia tour yake.


                                                           Lady Gaga

No comments:

Post a Comment