huko mjini Abidjan konda aliamua kumfokea mwanamke mnene kua anachukua nafasi kubwa ya watu wawili anakaa yeye mwenyewe, hivyo kama anataka apande! basi alipe nauli ya watu wawili,anasimulia mchoraji wa picha hiyo hapo juu aitwae Augustin Kassi.
baadhi ya tamaduni hapa ulimwenguni hususani Ghana na Ivory Coast wanawaheshimu sana wanawake wanene kwani wanatoa ishara kwamba waume zao wanawatunza vyema na miili yao imeonesha shukrani tena akiisha pata mtoto waume hushughulika kulisha vyema wake zao ili watokapo kwenye arobaini baada ya kujifungua basi wawe wamebadili , hili limeenea sana Mkoani Kilimanjaro na mtazamo kama huo wa kupenda wanwake wanenen kwa hapa Kwetu Tanzania uko mkoa wa Mbeya.
wachoraji wa mambo ya maumbile, wanajivunia sana kuchora marembo ya dunia ikiwemo maua, mimea,wanyama, na wanaona fahari kuona viumbe vyote vinaishi kwa amani.maonesho hayo yamefanyika mwezi huu wote huko Abidjan Ivory Coast ambayo yalihusisha michoro ya kipekee ni wanawake wenye maumbile manene,Augustin Kassi ambaye ni mchoraji mashuhuri nchini Ivory Coast akiwa na nia ya kubadilisha dhana ya kuwadharau wanwake wanene ambao mara kwa mara wanachekwa kutokana na taswira yao, na yeye ameamua kundaa maonesho hayo kwa kumuiga roll model wake mchoraji kutoka nchini Uingereza Beryl Cook .
Kassi anasema muhimu ni kuwapa moyo wanawake wanene badala ya kuwacheka na kuwadharau.
Augutine Kassi- mchoraji na mwanaharakati wa kutetea wanawake wanene, hahahahha
No comments:
Post a Comment