Tuesday, May 29, 2012

Ubaguzi wa rangi katika sanaa Ulaya



Kama ulidhani ubaguzi wa rangi umekwisha! basi utakua umejisahaulisha kidogo tu! kwa maifa machache na watu wachache wenye ubinafsi uliopindukia wanauendeleza ubaguzi wa rangi. kuna shindano la kisanii linaloelekea kwenye kilele nalo linalenga kusherehekea usanii wa kitsch (barani Uropa),  shindano hilo  la muimbaji bora la Eurovision kila linapofanyika huzua hisia za kichochezi ambazo sio kawaida kutokea kwingineko.
Na hivyo ndivyo ilivyo mwaka huu wakati shindano hilo likielekea kileleni. Hisia za ubaguzi wa rangi tayari zimeanza kuzungumziwa kabla ya shindano hilo kufikia fainali.
Chama chenye msimamo mkali cha Freedom Party, nchini Ukrain, kilimshambulia kwa maneno msanii Gaitana - ambaye ni mzaliwa wa Congo na ambaye anawakilisha Ukraia kwenye shindano hilo.







"Mamilioni ya watu watakaokuwa wanatizama fainali ya shindano hilo, watajionea Ukraian ikiwakilishwa na mtu ambaye sio wa rangi yetu" ndivyo alivyosema Yuri Syrotyuk, ambaye chama chake kianajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge baadaye mwaka huu."Ukrain itaonekana kama nchi iliyo katika eneo la vijijini huko barani Afrika" aliongeza kusema Yuri Syrotyuk,
Hata hivyo baadaye alikana madai ya ubaguzi wa rangi, akisema kuwa alikuwa anakosoa tu kutokuwepo uwazi katika namna mwakilishi kutoka nchini humo alivyochaguliwa.
Lakini matamshi yake yalikemewa sana nchini Ukraine na vyama vyote rasmi vya kisiasa na wasanii wengine mfano Vitaly, Volodymyr Klitschko na mshindi wa shindano hilo mwaka 2004, Ruslana.



Gaitana, atamenyana na wenzake katika awamu ya nusu fainali Alhamisi usiku, na amesema kuwa matamashi hayo ya ubaguzi wa rangi yameonyesha tatizo hilo lilivyokithiri nchini Ukraine.
"Nimekerwa sana na matamshi hayo, kwa sababu Ukrain ni nchi yenye demokrasia ambako watu wenye unyenykevu na utu wanaishi" alisema Gaitana.
Babake Gaitana ambaye ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alisomea katika mji mkuu wa Ukrain, Kiev, ambako alikutana na mamake Gaitana na kumuoa.
Muda mfupi baada ya kuzaliwa kwa Gaitana, mwaka 1979, familia yake ilihamia Congo-Brazzaville ambako waliishi kwa miaka mitano. Hata hivyo wazazi wake walitalakiana lakini mamake Gaitana alirejea naye nchini Ukrain.




Gaitana huandika nyimbo zake mwenyewe na anajioana kama mchanganyiko wa tamamduni mbili kwa sababu marafiki zake nchini Congo wanasema mziki wake una mizizi ya Kiafrika.
Fainali ya shindano hilo itafanyika nchini Azerbaijan na kutazamwa na watu milioni 125 kote barani Uropa. Wengi wanaona kama Gaitana ana nafasi nzuri ya kushinda shindano hilo.Atamenyana na washindani kutoka nchini Sweden, Uturuki, Romania, Italia na Ugiriki.
ALL THE BEST GAITANA






No comments:

Post a Comment