Baadhi ya wachezaji wa Simba
Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC imetupwa nje ya michuano ya kombe la shirikisho Africa CAF kwa mikwaju ya penalti 9-8 na timu ya Al Ahly Shandy ya Sudan baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0 kwenye dakika 90 za mechi hiyo ya marudiano
Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba wameshindwa kuunguruma nchini Sudan na
kukubali kipigo cha mabao 3-0 toka kwa Al Ahly Shandy na baadae kutolewa kwa mikwaju ya penalti 9-8. Simba iliingia kwenye mechi hiyo ikiwa na ushindi wa mabao 3-0 iliupata kwenye mechi ya awali iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Simba, Emanuel Okwi alifunikwa kwenye mechi hiyo na alishindwa kabisa kuonyesha cheche zake kama ilivyokuwa kwenye mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam.
Simba iliweza kujilinda kwenye kipindi cha kwanza na haikuruhusu washambuliaji wa Al Ahly Shandy kuliona lango lake. Timu zote mbili zilienda mapumziko zikiwa 0-0.
Katika kipindi cha pili, Simba ilikubali kuruhusu magoli mawili ya haraka kwenye dakika ya kwanza na ya tatu ya kipindi cha pili.
Katika dakika ya 59 makosa ya Victor Costa yalipelekea mshambuliaji wa Al Ahly Shandy, Farid Mohammed kuipatia timu yake goli la tatu lililoizamisha kabisa vijana hao wa mtaa wa Msimbazi.
Mechi hiyo ilimalizika Simba ikiwa imelala 3-0 na mechi hiyo ikabidi iingie kwenye hatua ya mikwaju ya penalti.
Penalti 10 zilipigwa ambapo Simba walikosa penalti mbili zilizopigwa na Patrick Mutesa Mafisango na Juma Kaseja. Kaseja pia aliokoa penalti moja ya Al Ahly Shandy.
Kwa kipigo hicho, Simba imeliaga kombe hilo na kuiacha Al Ahly Shandy ikisonga mbele.
No comments:
Post a Comment