Monday, May 21, 2012

.Chelsea- Bingwa wa Ulaya 2012




 
            

muuaji wa Bayern Munich,mkwaju wake uliwafunga midomo washabiki wa timu hiyo.


Chelsea ya England imeshinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya 2012 baada ya kuwashinda Bayern Munich ya Ujerumani kwa mikwaju ya penati 4-3.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1 baada ya dakika 90 za kawaida na kulazimika kwenda katika dakika za nyongeza. Hata hivyo timu hizo ziliendelea kuwa sare na hivyo kulazimika kuamiliwa kwa mikwaju ya penati.


mahali kilipopigwa, Stamford Bridge

Awali, Thomas Muller alindika bao la kwanza kwa Bayern Munich katika dakika ya 83, lakini Didier Drogba alisawazisha kwa mpira wa kichwa katika dakika ya 88.
Mchezo uliendelea katika muda wa ziada na dakika nne za kipindi cha kwanza Drogba alimfanyia faulo Frank Ribery ndani ya eneo la hatari na kusababisha penati. Arjen Robben alipiga penati hiyo lakini ilidakwa na kipa Petr Cech. Maelfu kwa maelfu ya mashabiki wanaimba na kushangilia kikosi cha Chelsea kilichoshinda Ligi ya mabingwa baada ya kurejea kutoka Munich kupitia mitaa ya London ya magharibi.
Timu ya Chelsea ikisafiri juu ya mabasi mawili yaliyo wazi, ilianza msafara wake kutoka uwanja wa Stamford Bridge majira ya adhuhuri hapa London.
Chelsea au maarufu kama The Blues' ilifanikiwa kushinda kombe la Ligi ya mabingwa kwa kuibwaga klabu iliyo shinda kombe le mshindi mara nne, Bayern Munich huko Ujerumani.Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya London kushinda kombe la Ulaya.


Rahaaaaa

Basi ambalo Timu ya Chelsea ilisafiria, limepambwa kwa rangi za klabu, na limekua likisimama kwenye kila hatua ambapo wachezaji wakiliinua Kombe kuwaonyesha mashabiki waengi ambao wamekua wakijitokeza kwa masaa mengi.Mashabiki wamekua wakiwarushia wachezaji mawele kama ishara ya kuwaenzi -desturi iliyoanza mwishoni mwa miaka ya 1980, mashabiki walipoanzisha tabia ya kurusha figili angani, na kufuatiwa na nyimbo.
Baadaye klabu ya Chelsea ikapiga marufuku figili kutumiwa ndani ya uwanja wa Stamford Bridge.Mwandishi wa BBC aliyeshuhudia sherehe hizo Ed Davey, amesema kua mashabiki walirusha vijiti vya figili wakati wakisubiri msafara, lakini walikua wachangamfu waliojaa nidhamu.


                                                                            figili

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema si jambo la kawaida kuiona timu kutoka Uingereza ikishindana kupiga mashuti ya matuta dhidi ya klabu kutoka Ujerumani na Waingereza kushinda.
Nilishuhudia yote hayo nikiwa pamoja na Chancellor wa Ujerumani, ulikuwa wakati mgumu kusubiri kuona mshindi, lakini baadaye tulipongezana,alisema Waziri Mkuu.


waziri mkuu wa uingereza David Cameroon na kansela Angela Mekel  wakishuhudia mtanange wa kukata na mundu

No comments:

Post a Comment