Wednesday, May 2, 2012

Na katika Michezo!

Man City yarejea kileleni

Yaya
Yaya Toure aliisaidia City kuizaba United

Manchester City imechukua tena usukani wa ligi kuu ya England na kuongeza matumaini ya kunyakua ubingwa baada ya kuwachapa mahasimu wao Manchester United kwa 1-0.
Mpira wa kona katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza uliopigwa na David Silva uliunganishwa na nahodha Vincent Kompany na kumpita kipa David De Gea na kuandika ndio bao pekee lililodumu hadi mwisho.
Kipindi cha pili Manchester United walianza kwa kasi lakini Manchester City waligangamala na kuwadhibiti wageni.
Manchester City sasa wanaongoza ligi licha ya kuwa na pointi sawa na Man United, lakini wana idadi kubwa ya magoli.
Fergie
Wametupilia mbali usukani...... Meneja wa United, Alex Ferguson
Tofauti ya magoli kati ya timu hizo mbili ni 8.
Ushindi huu wa aina yake umekuja wakati ndoto za Manchester City za kuchukua ubingwa zikiwa zimekwisha fifia baada ya kufungwa na Arsenal mwanzo wa mwezi Aprili huku United wakiongoza kwa pointi nane.
Ligi hii huenda ikamalizika kwa chachu kubwa katika michezo miwili iliyosalia ambayo timu zote hazina budi kushinda iwapo zinataka kuweka matumaini ya kunyakua ubingwa.
Man City watakwenda kupambana na Newcastle kabla ya kuikaribisha QPR, huku United wakicheza na Swansea kwenye uwanja wa Old Trafford kabla ya kusafiri kupambana na Sunderland katika mchezo wa mwisho wa ligi.

No comments:

Post a Comment