Eugene Terre' Blanche
Polisi wameimarisha doria hii leo katika mji wa Ventersdorp, nchini Afrika Kusini ambapo mahakama inasubiriwa kutoa hukumu kwa vijana wawili wa Kiafrika wanaotuhumiwa kumuua Eugene Terre' Blanche miaka miwili iliyopita.
Bwana Terre' blance alikuwa kiongozi wa mrengo wa kulia wa vuguvugu la kupigania utawala wa kizungu la Afrikaan Resistance Movement.
Wanaharakati wengi wa kutoka vuguvugu hilo hii leo wanatarajiwa kupiga kambi nje ya mahakama hiyo wakiwa wamevalia sare za chama hicho na wamebeba bunduki.Polisi wamejitayarisha kupambana na ghasia
Chris Mahlangu mwenye umri wa miaka 28, na mvulana mmoja ambaye hawezi kutajwa kwa sababu ya umri wake, wanakabiliwa na mashtaka ya kumpiga aliyekuwa kiongozi wa AWB, Eugene Terreblance, hadi kufa nyumbani kwake viungani mwa mji wa Ventersdorp miaka miwili iliyopita.
Chris Mahlangu
Wawili hao wamekanusha mashtaka ya kumuua muajiri wao na kutekeleza uwizi wa mabavu.Mahlangu anadai kuwa alikuwa akijitetea ili hali mvulana anayeshtakiwa pamoja naye amekanusha kuhusika na uhalifu huo.
Kizingiti kikubwa katika kesi hii ni kuwa Mahlangu na mvulana huyo walikataa kutoa ushahidi wao, wakati wa kesi hiyo.Hali ya wasi wasi inatarajiwa kutanda nje la makahakama hiyo kama ilivyokuwa wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo miaka miwili iliyopita.
Wakati huo, polisi walikabiliwa na wakati mgumu kuwatenganisha makundi ya wafuasi wa pande hizo mbili.Lakini idara ya polisi na chama cha AWB zimesema kuwa ghasia zozote hazitarajiwi.
Polisi wamesema ikiwa mambo yatakwenda kinyume na matarajio yao, imeweka mikakati thabiti ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote atakayevuruga shughuli za mahakama.Mwezi uliopita, wakati mawakili walipokuwa, wakitoa tetesi zao za mwisho mbele ya mahakama hiyo, jaji alionya kuwa hukumu huenda ikachukua muda mrefu lakini haijulikani, ikiwa uamuzi huo utachukua zaidi ya siku moja kutolewa.Hata hivyo pande zote zinatarajiwa kukata rufaa baada ya hukumu kutolewa.
No comments:
Post a Comment