Marehemu Patrick Mafisango
Kwa taarifa zilizotufikia muda huu zinaeleza kuwa kiungo mkabaji wa wa timu ya SIMBA SPORTS CLUB PATRICK MAFISANGO amefariki dunia alfajiri ya leo.
Mchezaji huyo amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika eneo la CHANGOMBE jijini DSM
Ikumbukwe kuwa PATRICK MAFISANGO alijiunga na Klabu ya SIMBA katika msimu huu wa ligi ambayo imeisha hivi karibuni akitokea AZAM
Kwa taarifa zaidi endelea kusikiliza Clouds fm kupitia Power Break fast kwa taarifa zaidi na wakati huo huo CLOUDS MEDIA GROUP inatoa pole kwa ndugu ,jamaa na marafiki pamoja na mashabiki wote wa soka nchini
No comments:
Post a Comment